Nafasi Ya Matangazo
Showing posts with label AFYA YAKO. Show all posts
Showing posts with label AFYA YAKO. Show all posts

January 19, 2018

Mwandishi Wetu, TJNCDF
Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza Tanzania (TANCDA) linaeleza kuwa karibu kila mtu anakabiliwa na tatizo la msongo wa mawazo.

Kinachosababisha hali hiyo, TANCDA inaeleza kuwa ni hali ya jumla ya maisha. Mazingira na mifumo ya maisha ambayo jamii inaishi yanachagiza binadamu kujikuta anapata msongo wa mawazo.

Kuna mambo mengi yanayoweza kumsababishia mtu kuwa na msongo, na hapa TANCDA inayaelezea kwa mfumo wa maswali.

Katika maswali hayo ukiona miongoni yanakuhusu, unapaswa kuchukua tahadhari ili tatizo la msongo wa mawazo lisikusababishie madhara.

Siyo rahisi mtu kujua madhara anayopata kama yanatokana na msongo wa mawazo yanayomkabili kwa sababu hiyo TANCDA inashauri jamii kuchukua tahadhari.
Miongoni mwa maswali mtu anayoweza kujiuliza ni: Je, hatuwi na wasiwasi kuwa watu wanachunguza ngua tunazovaa?

Je, hatushikwi na hofu pale tunapovuka barabara kuwa tunaweza kugongwa na magari? Je, hatuwi na wasiwasi pale tunaposhindwa kumaliza kazi zetu kwa wakati? BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI MAKALA HAYA.
Posted by MROKI On Friday, January 19, 2018 No comments
Mwandishi Wetu, TJNCDF

Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza Tanzania (TANCDA) linaeleza kuwa moyo na mishipa ya damu ni mfumo wa kusambaza na virutubisho mwilini.

Madhara hutokea iwapo nguvu inayosukuma damu itakuwa juu zaidi ya kawaida na kusababisha shinikizo la damu. Madhara mengine ni kuziba kwa mishipa ya damu.

TANCDA inaeleza kwamba msukumo ukiwa juu sana unaweza kusababisha moyo kushindwa kupiga, kupasuka kwa mishipa ya damu na kusababisha kiharusi au kifo cha ghafla.

Madhara mengine yanayoweza kutokea, yanaelezewa na TANCDA kuwa ni figo kushindwa kufanya kazi.

Mazingira yanayoweza kusababisha mishipa ya damu kuziba inaelezwa kuwa ni mafuta kuzidi katika mfumo wa damu.

Mafuta yanayoweza kusababisha mazingira hayo, TANCDA inayataja kuwa ni yale yanayotokana na wanyama kwani ni rahisi kuganda kusababisha athari kwenye mishipa. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI MAKALA HAYA 
Posted by MROKI On Friday, January 19, 2018 No comments
Mwandishi Wetu, TJNCDF

Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza Tanzania (TANCDA) limetoa maelekezo muhimu kwa jamii katika kufanikisha suala zima la kuepuka au kudhibiti magonjwa sugu.

Magonjwa sugu yanayoelezewa na TANCDA ni yale yasiyo ya kuambukiza na ikajikita kwenye magonjwa manne makuu ambayo yamekuwa yanawasumbua wengi, hasa katika nchi masikini.

Magonjwa hayo sugu ni: Moyo na mishipa ya damu, njia ya hewa na mapafu, kisukari na saratani.

Makamu Mwenyekiti wa TANCDA, Profesa Andrew Swai anasema kuwa kutibu magonjwa haya kunatumia fedha nyingi hivyo anaishauri jamii kuchukua tahadhari ya kuepukana nayo.

Kwa wale ambao tayari wameambukizwa, Profesa Swai anasema wanapaswa kufuata kikamilifu maelekezo ya madaktari hospitalini ili kuyadhibiti kikamilifu.

Zipo njia nyingi za kukabiliana na magonjwa haya lakini kwa hapa TANCDA inatoa elimu juu ya mtindo bora wa maisha kwa kupangilia vizuro mipango ya mlo na kuhakikisha chakula unachotumia ni cha kuboresha afya. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI MAKALA HAYA.
Posted by MROKI On Friday, January 19, 2018 No comments
Mwandishi Wetu, TJNCDF

Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza Tanzania (TANCDA) limekuwa likitoa elimu kwa ajili ya kuelimisha jamii juu ya magonjwa sugu.

Lengo ni kuiwezesha jamii kuwa na elimu sahihi juu ya namna ya kuyaepuka au njia sahihi za kuyadhibititoa kwa wale ambao tayari wameathirika.

TANCDA inaamini kwamba jamii ikiwa na uelewa wa magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza ni namna sahihi ya kuiokoa jamii ya sasa na vizazi vijavyo.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa kadri miaka inavyoongezeka kasi ya watu kupata magonjwa haya inaongezeka na inasababisha adha nyingi zikiwamo kupunguza nguvu kazi, kutumia raslimali nyingi za fedha na kusababisha vifo.

Magonjwa sugu ya mfumo wa hewa ni miongoni mwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo TANCDA inayawekea kipa umbele katika kuielimisha jamii.
§1
TNCDA katika moja ya vipeperushi vyake vya kuielimisha jamii, inaeleza kuwa magonjwa sugu ya mfumo wa hewa na mapafu hutokana na kuziba kwa njia ya hewa na kusababisha mtu apumue kwa shida.

Inaeleza kwamba kwa kawaida mtu anapozaliwa kinga ya mwili inakuwa na mfumo wa kuzoea vitu kwenye mazingira yetu na kuishi navyo bila shida.

Sababu moja ya pumu ni hali ambapo uzoefu na vitu kadhaa haukutosha hivyo kusababisha njia ya hewa kuchukua tahadhari ambazo madhara yake ni kuziba kwa njia ya hewa. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI MAKALA HAYA
Posted by MROKI On Friday, January 19, 2018 No comments

January 18, 2018

Mwandishi Wetu
WATU wengi wamekuwa wakipata matatizo ya meno na hata kulazimika kung'oa bila kujua tatizo hilo linatokana na nini na ni namna gani ya kulikabili.

Wengine hujikuta wakitangatanga huko na kule na hata kwenda kwa waganga wa kienyeji lakini matokeo yake tatizo huzidi kuwaandamba.

Ili kujua hatua ambazo unapaswa kuzichukua Dkt. Onesmo Kapugi anaanza kwa kueleza nini maana ya kutoboka kwa meno.

Kutoboka kwa meno ni ile hali ya jino au meno kutengeneza tundu ikiwa ni matokeo ya asidi (tindikali) izalishwayo na bakteria baada ya mtu kula vyakula vyenye sukari.

Meno kutoboka husababishwa na tindikali izalishwayo na bakteria walioko kwenye utando mlaini ambayo taratibu huweza kutoboa jino husika kwa kuanzia kwenye tabaka la nje kabisa la jino na kuzidi kuingia ndani. Kutoboka kwa jino huharibu jino husika ambalo lisipozibwa mapema huweza kuishia kung’olewa.

Meno hutoboka wakati sukari iliyopo kwenye chakula inapotumiwa na bakteria walioko kwenye kinywa ambao kisha hutengeneza tindikali (asidi). 

Kila mara ulapo ama unywapo vitu vilivyo na sukari, tindikali hii hushambulia meno na taratibu huweza kuyatoboa. 

Mashambulizi haya huweza kuchukua hata saa moja baada ya kuwa umekula vitu vya sukari. Ikumbukwe kuwa si sukari tu ambayo ni tishio kwa meno yako, hata vyakula vya wanga navyo ni hatari kwani vinaposagwa huweza kutoa sukari ambayo nayo huchangia kuozesha meno. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI MAKALA HAYA.
Posted by MROKI On Thursday, January 18, 2018 No comments

Mwandishi Wetu
KISUKARI ni ugonjwa unaoonyesha viwango vikubwa vya glukosi katika damu. Sababu yake ni uhaba wa homoni ya insulini mwilini au upungufu wa uwezo wa mwili wa kukubali insulini.

Kuna watu wanaozaliwa wakiwa hawana insulin hiyo inayochochea matumizi ya sukari, hivyo kuwa na kisukari cha utotoni na kuna wanaokipata kutokana na mwenendo wa tabia za maisha.

Vile vile, kuna wanawake wanaokipata wakati wakiwa wana mimba lakini baada ya kujifungua hupana na mwili wao unarejea katika hali ya kawaida.

Kwa ujumla ugonjwa wa kisukari hutokana na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kuliko inavyotakiwa au kuna mkwamo wa matumizi mwilini. Sukari kwenye damu ikizidi viwango vya kawaida kwa muda mrefu husababisha madhara mengi mwilini.

Chama cha Ugonjwa wa Kisukari (TDA) katika taarifa yake juu ya “nini ufahamu kuhusu ugonjwa wa kisukari’ kinasema sukari mwilini hutokana na vyakula pamoja na vinywaji ambavyo mtu anavitumia kila siku na kazi yake kubwa ni kuupa mwili nguvu.

Athari za ugonjwa wa kisukari
Ugonjwa wa kisukari unasababisha athari nyingi mwilini. Miongoni ni pamoja na magonjwa ya moyo kuwa zaidi ya mara mbili zaidi ya watu wasio na ugonjwa huo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI MAKALA HAYA.
Posted by MROKI On Thursday, January 18, 2018 No comments
Mwandishi Wetu
AKIWA amelazwa katika Taasisi ya Taifa ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), iliyopo jijini Dar es Salaam anaeleza kuwa afya yake imedhoofu sana ukilinganisha na hali halisi aliyokuwa nayo miaka mitatu iliyopita.
Crisent Bagara (62) anasema baada ya uchunguzi madaktari wa ORCI wanasema anasumbuliwa na saratani ya koo iliyotokana na uvutaji wa sigara.
Bagara anasema anahisi kushiwa nguvu, hawezi kumeza chakula na familia yake kwa sasa imeathirika kiuchumi kutokana na gharama kubwa za matibabu ya saratani.
Bagara ambaye kwa sasa anapata tiba ya mionzi anasema anajuta kujiingiza kwenye matumizi ya sigara kwa kuwa licha ya kumuathiri kiafya kwa muda mrefu imemrejesha kwenye umaskini.
“Nilikuwa mkulima wa mahindi, maharagwe, alizeti na mazao mbalimbali eneo la Oldian, wilaya ya Karatu, mkoani Arusha. Nilipata fedha nyingi, nimesomesha watoto hadi sasa wanajitegemea na sikuwahi kupata shida ya kifedha,” anasema.
Tangu ameanza kuumwa miaka mine iliyopita anasema kidogokidogo kasi yake ya kujiingiza kwenye kilimo ilipungua. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI MAKALA HAYA.
Posted by MROKI On Thursday, January 18, 2018 No comments
Mwandishi Wetu
Wataalamu wa afya wanasema sigara haina manufaa yoyote kwa binadamu zaidi ya kuathiri afya na yeyote anayetumia tumbaku anawekwa kwenye kundi la wagonjwa.

Wavutaji wengi wa sigara wanafahamu sigara zina madhara mengi ya kiafya lakini si rahisi kwao kuziacha kwa vile wanajihisi bila kuvuta hawana uwezo wa kutekeleza kazi zao kikamilifu.

Kwa miaka mingi, wataalamu wamebaini kuwa pamoja na tumbaku kuwa na viambata vingi, kinachochochea hamu ya mara kwa mara (uraibu) ya uvutaji wa sigara ni kemikali aina ya nikotini.

Dk Ananya Mandal wa Chuo Kikuu cha Afya cha West Bengal nchini India anasema mtu anapovuta sigara, moshi wake huandamana na kemikali ya nikotini hadi kwenye mapafu na kunyonywa na vifuko vya hewa ambavyo huiingiza kwenye mfumo wa damu.

Katika makala yake aliyoiandika na kuchapishwa na Jarida la News Medical, Dk Mandal anasema iwapo mtu atakuwa anatafuna tumbaku, nikotini itakuwa inafyonzwa na ngozi laini puani na kuingizwa kwenye mfumo wa damu. 

Nikotini inapokuwa kwenye mfumo wa damu husafiri hadi kichwani na kuachana na mishipa ya damu na kuingia kwenye ubongo.

Uchunguzi wa kisayansi umebaini kuwa nikotini baada ya kuingia kwenye mfumo wa damu si chini ya sekunde saba inakuwa imeufikia ubongo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI MAKALA HAYA.
Posted by MROKI On Thursday, January 18, 2018 No comments
Mwandishi wetu
MARA nyingi katika jamii kumekuwepo na neno linalotumiwa la ‘presha’ likiwa na maana wasiwasi na kutojiamini. Na hii imekuwa ikitumika pale mtu anapokabiliwa na wakati mgumu kwa jambo fulani.

Sawia na matumizi hayo, kuna pia wanaoelezewa kuwa wanaugua presha na wanatumia dawa. Namna neno hilo linavyotumiaka yawezekana likawa linasababisha utata.

Hata hivyo, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Kituo cha Utafiti Tukuyu mkoani Mbeya inaeleza kwamba unapozungumzia kuhusu presha unaimanisha shinikizo la damu au wengine hufupisha kwa neno ‘BP’, ikiwa ni kifupi cha maneno ya kiingereza ya ‘Blood Presure.’

Maana ya Shinikizo 
NIMR inasema kuwa shinikizo au presha ni kipimo cha damu ambacho kinapima nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ya damu wakati moyo ukidunda. 

Kwa kawaida mtu anapopimwa huainishwa kwa vipimo viwili; presha ya systole na diastole.

Systole ni kipimo cha juu mfano 140 mm Hg ambacho hupima nguvu ya msukumo wakati moyo unadunda kusukuma damu.

Shinikizo au presha ya diastole ni kipimo cha damu ambacho kinapima nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa wakati moyo umepumzika au kati ya mapigo ya moyo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI MAKALA HAYA
Posted by MROKI On Thursday, January 18, 2018 No comments
Mwandishi Wetu

JUHUDI za kisayansi zinazofanywa kila kukicha ni kuwezesha binadamu kuishi maisha marefu duniani. Juhudi hizo siyo tu za binadamu kuishi maisha marefu bali kuwa na afya njema kwa maana ya kutokuwa na maradhi.

Maradhi hudhoofisha mwili na kuuweka kwenye hatari ya kupoteza uwezo wake wa kulinda uhai. Juhudi kubwa zinazofanywa na wataalamu wa afya kupitia tafiti mbalimbali ni kumuuweka mwili katika mazingira ya kujikinga na magonjwa, hasa yasiyo ya kuambukiza.

Hatua nyingine ni ya tiba au kudhibiti magonjwa ili yasiathiri mwili na kuuweka katika mazingira ya kushindwa kulinda uhai. Hii ni ya muhimu ili kuwasaidia wale ambao kwa bahati mbaya mipango ya kujikinga imeshindikana. Mikakati yote hiyo ni kulinda uhai ili binadamu aishi kwa muda mrefu.


Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yapo mengi, miongoni ni shinikizo la damu, kisukari, pumu, athari za viungo kama moyo, figo, ini, kinywa na ubongo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI MAKALA HAYA.
Posted by MROKI On Thursday, January 18, 2018 No comments

Mwandishi Wetu
WAGONJWA wengi wenye tatizo la shinikizo la damu hushindwa kufanya mazoezi ya mwili kutokana na ukweli kwamba, yanalazimisha moyo kufanya kazi ya ziada.

Wagonjwa wengi wa moyo wanapojaribu kufanya mazoezi, hukabiliwa na uchovu pamoja na kushindwa kuongeza pumzi.

Dalili hizi huwafanya wengi wao kuishi bila kuushughulisha mwili, jambo ambalo huathiri zaidi afya zao, mipango yao ya kiuchumi na ubora wa maisha kwa ujumla.
Ingawa mazoezi hufikiriwa kuwa ni hatari kwa wagonjwa wenye maradhi ya moyo, tafiti za hivi karibuni zinabainisha kuwa mazoezi ni muhimu sana kwa watu wenye maradhi haya.

Tafiti za kitabibu zinaonesha kuwa, mazoezi huwasaidia wagonjwa wa moyo kutumia hewa ya oksijeni vizuri na kwa faida.

Mazoezi pia huongeza mzunguko wa damu katika misuli mwilini na hupunguza kiasi cha lehemu mbaya mwilini, uwezekano wa kupata magonjwa yatokanayo na uvimbejoto, uwezekano wa kulazwa hospitalini mara kwa mara, matumizi ya dawa na vifo vya mapema.

Hii ni kwa mujibu wa Julie Adsett na Robbie Mullins wa Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Queensland cha Uingereza, katika chapisho lao la ushahidi wa kisayansi kuhusu faida za mazoezi kwa watu wenye maradhi ya moyo ya muda mrefu, lililotolewa mwaka 2010.

Katika makala yake iliyochapishwa katika jarida la Chama cha Madaktari wa Marekani (JAMA) toleo la 288(16) la mwaka 2002, Dk. Jonathan Myers (PhD) wa kitengo cha magonjwa ya moyo katika Chuo Kikuu cha Stanford nchini Marekani, anasema kwamba wagonjwa wapya wanaogunduliwa kuwa na shinikizo la damu, wanapata nafuu haraka wanaposhiriki katika mazoezi. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI MAKALA HAYA.
Posted by MROKI On Thursday, January 18, 2018 No comments
Mwandishi Wetu
SARATANI ya Shingo ya kizazi imekuwa tishio kwa wanawake wengi hapa nchini. 

Takwimu za mwaka 2016 zinaonesha kuwa asilimia 33 ya wanawake wenye saratani, wanaugua ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.

Mkurugenzi wa Idara ya Kinga ya Saratani katika hospitali ya Saratani Ocean Road, Dkt. Crispin Kahesa anasema kuwa

Dkt. Kahesa anasema saratani ya shingo ya kizazi ni kati ya magonjwa yanayosababisha wanawake wengi kupoteza maisha kwa kutofahamu uwepo wa tatizo hilo.

Anasema saratani ya shingo ya kizazi imeshika nafasi ya pili kwa magonjwa ya saratani kwa wanawake na ni sababu kubwa ya vifo vya wanawake katika nchi zinazoendelea.

Saratani hii husababishwa na virusi viitwavyo 'Human papilloma Virus (HPV)’ iwapo kinga ya mwili itashindwa kuondoa maambukizi ya hivi virusi. 

Dkt. Kahesa anasema iwapo maambukizo hayo yataendelea kwa muda mrefu chembe hai za kawaida huanza kukua bila mpangilio na kuwa saratani, jambo ambalo linaweza kuchukua miaka miwili hadi ishirini tangu kuambukizwa.

Kirusi cha HPV huenea kwa njia ya kugusana sehemu za siri, hivyo maambukizo yanaweza kutokea hata kama tendo la kujamiina halijahusisha muingiliano wa sehemu za siri. Hivyo mpira wa kiume unaweza kupunguza maambukizi lakini si kwa asilimia 100. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI MAKALA HAYA.
Posted by MROKI On Thursday, January 18, 2018 No comments
Mwandishi Wetu 
KINYWA ni moja ya viungo muhimu katika mwili wa binadamu hasa ikizingatiwa kwamba kinatumika kula, kuzungumza, kuhisi na ni sehemu ya uzuri wa sura ya mtu.

Kutoboka meno na kuharibika fizi vyote vinaweza kuathiri baadhi ya sifa za kinywa, kumfanya mtu atumie fedha nyingi kwa matibabu na hata kuathiri muonekano halisi wa mtu.

Mfano mzuri ni kwamba mtu aking’oa meno mengi mdomoni anaweza akaathiri muonekano mzuri wa mdomo na mashavu, kushindwa kutafuna na hata kutamka maneno vizuri, na asipokuwa mwangalifu katika kusafisha kinywa pia anaweza kuwa anatoa harufu mbaya mdomoni.


Kuoza meno ni nini?

Ushirika wa Vyama Vinavyokabili Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza (TANCDA) katika kuelimisha jamii juu ya magonjwa ya kinywa inaeleza kuwa kuoza kwa meno ni hali ya sehemu ya juu ndani ya jino kutoboka kutokana na ulaji wa mara kwa mara wa vyakula vyenye sukari.

Taarifa hiyo ya TANCDA inasema vijidudu vya bakteria humeng’enya mabaki vya vyakula vya sukari mdomoni na kutoa tindikali ambayo husababisha kudhoofu kwa sehemu ya nje ya meno na baadae hutoboka.

Takwimu zinaonyesha kati ya asilimia 60 hadi 90 ya watoto wote wenye umri wa kwenda shule duniani kote wana ugonjwa wa meno kutoboka.

Hapa nchini, watoto wenye umri kati ya miaka mine hadi sita, mtoto mmoja kati ya watatu ana jino lililotoboka au kuoza.

Vyakula vinavyochochea bakteria kuathiri meno ni biskuti, soda, keki, chokoleti, pipi, kashata, aisikrimu, visheti na ubuyu wenye sukari. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI MAKALA HAYA.
Posted by MROKI On Thursday, January 18, 2018 No comments
Mwandishi Wetu
Wataalamu wa afya wanasema sigara haina manufaa yoyote kwa binadamu zaidi ya kuathiri afya na yeyote anayetumia tumbaku anawekwa kwenye kundi la wagonjwa.

Wavutaji wengi wa sigara wanafahamu sigara zina madhara mengi ya kiafya lakini si rahisi kwao kuziacha kwa vile wanajihisi bila kuvuta hawana uwezo wa kutekeleza kazi zao kikamilifu.

Kwa miaka mingi, wataalamu wamebaini kuwa pamoja na tumbaku kuwa na viambata vingi, kinachochochea hamu ya mara kwa mara (uraibu) ya uvutaji wa sigara ni kemikali aina ya nikotini.

Dk Ananya Mandal wa Chuo Kikuu cha Afya cha West Bengal nchini India anasema mtu anapovuta sigara, moshi wake huandamana na kemikali ya nikotini hadi kwenye mapafu na kunyonywa na vifuko vya hewa ambavyo huiingiza kwenye mfumo wa damu.

Katika makala yake aliyoiandika na kuchapishwa na Jarida la News Medical, Dk Mandal anasema iwapo mtu atakuwa anatafuna tumbaku, nikotini itakuwa inafyonzwa na ngozi laini puani na kuingizwa kwenye mfumo wa damu. 

Nikotini inapokuwa kwenye mfumo wa damu husafiri hadi kichwani na kuachana na mishipa ya damu na kuingia kwenye ubongo.

Uchunguzi wa kisayansi umebaini kuwa nikotini baada ya kuingia kwenye mfumo wa damu si chini ya sekunde saba inakuwa imeufikia ubongo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI MAKALA HAYA.
Posted by MROKI On Thursday, January 18, 2018 No comments
Mwandishi wetu
TAFITI mbalimbali za hapa nchini zinaonyesha kuwa watu wengi wanaougua saratani huwa hawajifahamu hadi hali zao zinapokuwa mbaya.

Taarifa ya Taasisi ya Taifa ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) inaeleza wagonjwa wengi hufikishwa katika hospitali hiyo wakiwa katika hali mbaya na wengine huwa ni vigumu kupona.

Wanaeleza ya kuwa ni ukweli kwamba saratani nyingi zinaweza kutibiwa kirahisi iwapo mgonjwa atawahi kupata matibabu.

Hii ndiyo kusema elimu ya ugonjwa huo ni ya msingi sana katika kuwafanya watu wawahi hospitali mapema wanapoona dalili za saratani.

Kulingana na wataalamu wa afya, saratani ni ugonjwa unaosababishwa na seli za eneo fulani la mwili kubadili tabia na kuzaliana kwa kasi bila mpangilio na kuathiri utendaji wa mwili.

Zipo saratani za aina nyingi na kila moja ina dalili zake. Mfano ni saratani ya koo, ubongo, damu, kibofu cha mkojo, shingo ya kizazi, matiti na ngozi.

Takwimu za ORCI zinaonesha kuwa idadi ya wagonjwa wapya wa saratani wanaofika kutibiwa inaongezeka kila mwaka.

Taarifa za serikali zinaeleza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoendelea zinazoongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi wa saratani za njia ya mfumo wa chakula na ini, ikilinganishwa na nchi nyingine. BOFYA HAPA KUSOMA MAKALA HAYA ZAIDI
Posted by MROKI On Thursday, January 18, 2018 No comments

January 17, 2018


Mwandishi Wetu

AFYA bora ya kinywa na meno kwa mtoto ni muhimu na ina uhususiano wa moja kwa moja na afya yake kwa ujumla. Utunzaji huu unatakiwa kuanza na meno ya utotoni

Wazazi au walezi wengi wamekuwa wakijiuliza kwa nini wahangaike kutunza meno ya utotoni ambayo yanatarajiwa kung’oka?

Katika mahojiano na Daktari wa afya ya kinywa na meno, Dk Frank Mbaga anasema meno ya utoto ni muhimu kwa kuwa hali mbaya ya afya ya meno ya utotoni huathiri hali ya afya ya meno ya ukubwani, humzuia mtoto kutafuna vizuri na hushindwa kutunza nafasi kwa ajili ya meno ya ukubwa.

Madaktari wa afya ya kinywa na meno na watafiti wanakualiana kwamba mambo yanayochangia maamubukizo na ugonjwa wa kuoza na kutoboka meno mapema kwa watoto ni matumizi ya vitu vyenye sukari na matumizi ya chupa za chuchu ya maziwa.

“Tatizo la utobokaji wa mapema wa meno ya watoto linatisha kwa sababu linaonekana kama ni ugonjwa wa kawaida, na limekuwa likiongezeka kwa kasi zaidi kwa watoto wadogo.”

Takwimu za Tinanoff & O`sullivan za mwaka 1997 zinaonyesha kuwa asilimia 90 ya watoto wenye umri kati ya miaka 3-5 wanatatizo hili. Na katika nchi zinazoendelea hali ni mbaya kwani ni asilimia 70. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI MAKALA HAYA 
Posted by MROKI On Wednesday, January 17, 2018 No comments
Mwandishi Wetu

Tabia na mienendo ya watu kimaisha imekuwa ni sababu ya matatizo kwao binafsi, jamii na hata kwa uchumi wa nchi, ambao unahitaji sana nguvu kazi inayotokana na afya njema.

Afya ya mtu yeyote inategemea sana namna anavyokula, anavyoishi na kujiweka katika mazingira yanayomzunguka ili kujikinga na maradhi.

Miongoni mwa mambo yanayohatarisha afya za watu wengi nchini ni ulaji usiofaa, kutokufanya mazoezi au kazi ngumu, utumiaji wa tumbaku, vileo na vipodozi visivyo salama. 

Tabia nyingine mbaya kwa afya ni uchafuzi wa mazingira, hewa, maji na uzalishaji wa makelele yasiyokuwa ya lazima.

Mambo mengine ni ile hali ya mtu kujiweka katika mazingira hatarishi kiusalama kama vile ngono zembe na mwendo kasi wa vyombo vya usafiri kiasi cha kuweza kusababisha ajali na kujeruhiwa au kufa.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa magonjwa yasiyoambukiza yanaongezeka kwa kasi katika jamii ya Watanzania. 

Magonjwa hayo ni kama vile kisukari, maradhi ya moyo, saratani, magonjwa sugu ya njia za hewa na mapafu, ajali za barabarani na magonjwa ya akili. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI MAKALA HAYA.
Posted by MROKI On Wednesday, January 17, 2018 No comments
Mwandishi wetu
UGOJWA wa kisukari hutokana na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kuliko inavyotakiwa. Sukari kwenye damu ikizidi viwango vya kawaida kwa muda mrefu husababisha madhara mengi mwilini.

Chama cha Ugonjwa wa Kisukari (TDA) katika taarifa yake juu ya “nini ufahamu kuhusu ugonjwa wa kisukari’ kinasema sukari mwilini hutokana na vyakula pamoja na vinywaji ambavyo mtu anavitumia kila siku na kazi yake kubwa ni kuupa mwili nguvu.

Athari za ugonjwa wa kisukari
Ugonjwa wa kisukari unasababisha athari nyingi mwilini. Miongoni ni pamoja na magonjwa ya moyo kuwa zaidi ya mara mbili zaidi ya watu wasio na ugonjwa huo.

Matatizo mengine ni shinikizo la damu, kiharusi, kuharibika mishipa ya damu na ile ya fahamu kiasi cha kusababisha ganzi, vidonda na hata gangirini ya miguu. Takwimu zinaonyesha kwamba ugonjwa wa kisukari ni moja ya sababu za watu wengi kukatwa miguu.

Ugonjwa wa kisukari pia husababisha kuharibika kwa figo na kuzifanya kushindwa kufanya kazi. Pia husababisha matatizo ya macho na upofu.

Madhara mengine ni kupungua kwa kinga ya mwili na kuuweka mwili katika hatari ya maambukizi ya ngozi, fizi, njia ya mkojo, uke na kifua kikuu. Vile vile unaweza kusababisha kupungua nguvu za kiume, utendaji wa kazi na kuathiri uchumi. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Posted by MROKI On Wednesday, January 17, 2018 No comments
  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo