Nafasi Ya Matangazo

January 18, 2018

Mwandishi Wetu

JUHUDI za kisayansi zinazofanywa kila kukicha ni kuwezesha binadamu kuishi maisha marefu duniani. Juhudi hizo siyo tu za binadamu kuishi maisha marefu bali kuwa na afya njema kwa maana ya kutokuwa na maradhi.

Maradhi hudhoofisha mwili na kuuweka kwenye hatari ya kupoteza uwezo wake wa kulinda uhai. Juhudi kubwa zinazofanywa na wataalamu wa afya kupitia tafiti mbalimbali ni kumuuweka mwili katika mazingira ya kujikinga na magonjwa, hasa yasiyo ya kuambukiza.

Hatua nyingine ni ya tiba au kudhibiti magonjwa ili yasiathiri mwili na kuuweka katika mazingira ya kushindwa kulinda uhai. Hii ni ya muhimu ili kuwasaidia wale ambao kwa bahati mbaya mipango ya kujikinga imeshindikana. Mikakati yote hiyo ni kulinda uhai ili binadamu aishi kwa muda mrefu.


Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yapo mengi, miongoni ni shinikizo la damu, kisukari, pumu, athari za viungo kama moyo, figo, ini, kinywa na ubongo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI MAKALA HAYA.

Mtaalamu wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa Watoto, Dkt. Frank Manase anasema kutibu magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni gharama kubwa hivyo muhimu ni kuelimisha jamii kujikinga wasiyapate.
Hata hivyo, anasema kwa wale ambao tayari wameyapata wanapaswa kujitahidi kutekeleza maelezo ya kitaalamu ili wawe na afya njema na waishi muda mrefu.
Anasema magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni moja ya sababu za tishio la uhai wa binadamu duniani kwa sasa. 
“Kasi yake imekuwa ikiongezeka miaka hadi miaka. Hili ni tishio la kurejesha nyuma juhudi za kisayansi za kuhakikisha binadamu anaishi maisha marefu dunini,” anabainisha Dkt. Manase.
Katika kueleza mazingira hayo, Daktari Bingwa wa magonjwa ya figo, Dkt. Sanjay Maitra wa India aliwahi kunukuliwa akisema: “Kuishi ni jambo moja lakini kuishi maisha marefu yenye afya njema ni kitu kingine kabisa. 
“Hakuna anayeweza kuthibitisha ukweli huu zaidi ya wale wapatao adha itokanayo na  athari za magonjwa yasiyo ya kuambukiza.”
Anaelezea kuwa magonjwa hayo yanawaathiri watu wengi wazima kwa wadogo. Wengi wanaathirika na wanaoshindwa kuyakabili wanakuwa katika mazingira rahisi kufa.
Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanatokana na nini? Mwenyekiti wa Chama cha Ugonjwa wa Kisukari Tanzania (TDA), Profesa Andrew Swai anasema tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa hutokana na tabia za mienendo na ulaji mbaya.
Anasema mtu ambaye haushughulishi mwili kama sehemu ya mazoezi na anakula kwa wingi vyakula vyenye mafuta na wanga mwingi, anajiweka katika mazingira ya kupata magonjwa haya.
vifo kwa  wagonjwa hawa ni kushindwa kuyadhibiti. Kujenga mipango endelevu  ya matibabu kwa wagonjwa wa figo, moyo, kisukari, mfumo wa neva na uti wa mgongo  inaendelea kuwa changamoto nchini Tanzania.
Makala haya yameandaliwa na Chama cha Waandishi Wanaokabili Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (TJNCDF) kwa kushirikiana na Chama cha Ugonjwa wa Kisukari Tanzania (TDA). Maoni na ushauri tuma TJNCDF, S.L.P. 13695, Dar es Salaam.Posted by MROKI On Thursday, January 18, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo