Nafasi Ya Matangazo
Showing posts with label WAZIRI MKUU. Show all posts
Showing posts with label WAZIRI MKUU. Show all posts

January 31, 2024

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na  Mbunge wa Jimbo la Ismani William Lukuvi,  Bungeni jijini Dodoma, Januari 31, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na  Waziri wa Chi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama,  Bungeni jijini Dodoma, Januari 31, 2024. 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Det. Doto Biteko akiwasikiliza Waziri wa Chi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene na Mbunge wa Jimbo la Ismani William Lukuvi,  Bungeni jijini Dodoma, Januari 31, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Posted by MROKI On Wednesday, January 31, 2024 No comments

January 26, 2024

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mtawala wa Mamlaka ya Kusimamia Uendelezaji wa Mji wa Serik
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa zawadi Mtawala wa Mamlaka ya Kusimamia Uendelezaji wa Mji wa Serikali wa Korea Kusini, Hyeong Ryeol Kim alipozungumza naye kwenye Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam, Januari 26, 2024
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Mtawala wa Mamlaka ya Kusimamia Uendelezaji wa Mji wa Serikali wa Korea Kusini, alipozungumza naye kwenye Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam, Januari 26, 2024 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wasimamizi na wataalamu wa ujenzi wa Mji wa Serikali jijini Dodoma wahakikishe matarajio ya ujenzi huo yanafikiwa kama ilivyokusudiwa.
 
Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na Mtawala wa Mamlaka ya Kusimamia Uendelezaji wa Mji wa Serikali wa Korea Kusini, Mheshimiwa HyeongRyeol Kim.
 
Amekutana na kiongozi huyo leo Ijumaa, Januari 26, katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni Jijini Dar es Salaam, baada ya hafla ya utiaji saini mikataba ya makubaliano kati ya taasisi za Korea Kusini na Tanzania.
 
Makubaliano hayo yanahusu kubadilishana uzoefu juu ya usimamizi na uratibu wa uendelezaji wa makao makuu na mji wa Serikali pamoja masuala ya ujenzi vikiwemo viwanda, hoteli.
 
Utiwaji saini huo umefanyika kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi Uendelezaji wa Mji wa Segong na kampuni ya Heerim ya Korea Kusini katika masuala ya usanifu na ubunifu wa ujenzi kwenye Mji wa Serikali na Makao Makuu jijini Dodoma.
 
“Serikali ya Tanzania na Korea Kusini zina mahusiano mazuri ya kidiplomasia, hivyo matarajio yetu ni kuona Makao Makuu na Mji wa Serikali jijini Dodoma unakuwa mzuri.”
 
Kwa upande wake, Mheshimiwa HyeongRyeol Kim amesema utiaji saini wa makubaliano hayo ni fursa muhimu ya kuendeleza ushirikiano baina ya mataifa hayo.
 
Pia, Mheshimiwa Kim amemshukuru Waziri Mkuu kwa mapokezi mazuri aliyoyapata na amemuhakikishia kwamba nchi yao itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuliendeleza jiji la Dodoma.
 
Posted by MROKI On Friday, January 26, 2024 No comments

September 08, 2022

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Kikao na Viongozi wa Mkoa wa Tabora kwenye ukumbi wa Isike Mwanakinyungi  katika Manispaa ya Tabora, Septemba 8, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Kikao na Viongozi wa Mkoa wa Tabora kwenye ukumbi wa Isike Mwanakinyungi  katika Manispaa ya Tabora, Septemba 8, 2022.
Baadhi ya washiriki wa Kikao na Viongozi wa Mkoa wa Tabora wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao katika kikao hicho kwenye ukumbi wa Isike Mwanakinyungi katika Manispaa ya Tabora, Septemba 8, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Posted by MROKI On Thursday, September 08, 2022 No comments

September 05, 2022

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge na Uratibu, wakati alipokagua  maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Wizara mbalimbali katika Mji wa Serikali-Mtumba, Dodoma Septemba 05, 2022.
Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa majengo ya Wizara mbalimbali katika Mji  wa  Serikali - Mtumba jijini Dodoma . Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  alikagua ujenzi huo, Septemba 5, 2022. 

Posted by MROKI On Monday, September 05, 2022 No comments
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama makaravati wakati alipokagua mradi  wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya mzunguko wa nje  wa jiji la Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3  wakati alipokagua mendeleo ya ujenzi huo,  Septemba 4, 2022.  Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule na wa tatu kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatma Mganga.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitazama sampuli za udongo wakati alipotemblea maabara ya mradi wa ujenzi  kwa kiwango cha lami wa barabara ya mzunguko wa nje  wa jiji la Dodoma yenye urefu wa kilomita  112.3 ,  Septemba 4, 2022.  

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi  (Uchukuzi), Atupele Mwakibete wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya mzunguko wa nje  wa jiji la Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3,  Septemba 4, 2022. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza  Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS ) Mkoa wa Dodoma, Mhandisi  Salome Kabunda ( kulia) ambaye alikuwa akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi  kwa kiwango cha lami wa barabara ya mzunguko wa nje  wa jiji la Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3  wakati alipokagua mendeleo ya ujenzi huo,  Septemba 4, 2022. Wa pili kushoto ni  Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi  (Uchukuzi), Atupele Mwakibete na wa tatu kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu ) Caspar Mmuya.
Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje wa jiji la Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3 ambayo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake, Septemba 4, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi  (Uchukuzi), Atupele Mwakibete (wa pili kulia) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya mzunguko wa nje  wa jiji la Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3,  Septemba 4, 2022. Wa pili kushoto ni Mkuu w Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule na kulia ni Kaimu Meja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS ) Mkoa wa Dodoma, Mhandisi  Salome Kabunda. 
************
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakandarasi wa ujenzi wa mradi wa barabara ya mzunguko wa nje wa jiji la Dodoma kuongeza kasi ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati na kwa viwango.

 “Kazi inaendela vizuri, tunataka kazi ikamilike ikiwezekana hata kabla ya muda, Rais Samia Suluhu Hassan anatekeleza miradi hii ili iwanufaishe Watanzania, hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunasimamia na inakamilika kwa viwango na wakati”
 
Amesema hayo leo (Jumapili, Septemba 04, 2022) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa barabara ya mzunguko wa nje wa jiji la Dodoma. Mradi huo ni sehemu ya uendelezaji wa jiji hilo.
 
Pia, Waziri Mkuu amewataka Wahandisi Wasimamizi wa mradi huo wahakikishe wanasimamia kikamilifu wakandarasi ili barabara hiyo iweze kujengwa kwa viwango vilivyokubaliwa kwenye mkataba wa ujenzi wake.
 
Akizungumza na watanzania walioajiriwa katika mradi huo, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wawe walinzi wa vifaa vinavyotumika kwenye ujenzi na wahakikishe vifaa vinabaki salama “Pambaneni na wote wenye nia ya kuiba vifaa hivi, tunataka tupate barabara yenye viwango”
 
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ameitaka Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI kuweka utaratibu wa kuwaweka pamoja vijana ambao wanashiriki kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali nchini ili waweze kutumika zaidi kwenye makampuni ya ujenzi ya wazawa.
 
Kaimu Meja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS ) Mkoa wa Dodoma, Mhandisi  Salome Kabunda. amesema kuwa pamoja na mradi huo kusaidia kupunguza msongamano wa magari jiji la Dodoma pindi utakapokamilika, pia umesaidia kutoa ajira kwa wazawa zaidi ya 800.
 
“Mheshimiwa Waziri Mkuu utekelezaji wa mradi huu utawezesha kujengwa kwa vituo vya afya vinne katika mitaa ya Mahomanyika, Veyula, Nala na Ihumwa. Pia yatanunuliwa magari ya wagonjwa manne katika vituo hivyo”.
 
Aliongeza kuwa sehemu ya kwanza ya ujenzi wa barabara hiyo kutoka Nala-Veyula-Mtumba hadi bandari kavu ya Ihumwa (Km 52.5) unaojengwa kwa muda wa miezi 39, utagharimu shilingi bilioni 100.
“Sehemu ya pili ya ujenzi wa barabara hii kutoka Bandari kavu ya Ihumwa-Matumbulu hadi Nala (Km 60) unaojengwa kwa muda wa miezi 43, utagharimu shilingi bilioni 120.8 ”
 
Ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilimota 112.3 unafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)
Posted by MROKI On Monday, September 05, 2022 No comments

August 02, 2022

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kozi Fupi ya Kumi na Tatu ya Viongozi kwenye ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania,  mkoani Dar es Salaam, Agosti 2, 2022.
Baadhi ya washiriki wa   Kozi Fupi ya Kumi na Tatu ya Viongozi  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   wakati alipofungua kozi hiyo  kwenye ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania,  mkoani Dar es Salaam, Agosti 2, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri wanaoshiriki katika Kozi Fupi ya Kumi na Tatu ya Viongozi baada ya kufungua kozi hiyo kwenye ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania mkoani Dar es Salaam, Agosti 2, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax (wa pili kulia) na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja General Ibrahim Mhona (kushoto) baada ya kufungua   Kozi Fupi ya Kumi na Tatu ya Viongozi  kwenye ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania mkoani Dar es Salaam, Agosti 2, 2022. Wa pili kushoto ni Kansela wa Chuo cha Ulinzi Tanzania, Balozi Matern Lumbanga. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri wanaoshirki katika Kozi Fupi ya Kumi na Tatu ya Viongozi baada ya kufungua kozi hiyo kwenye ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania mkoani Dar es Salaam, Agosti 2, 2022. 
************
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka washiriki wa kozi fupi ya 13 ya viongozi watambue, wafuate na waisimamie falsafa ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan iliyojielekeza katika kuwahudumia watanzania.
 
Mheshimiwa Majaliwa amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwaongezea uelewa kuhusu masuala ya ulinzi na stratejia kwa ajili ya kulinda maslahi mapana ya Taifa katika utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku.
  
Waziri Mkuu amesema Serikali inatarajia kuona mabadiliko ya kimtazamo, ushauri na maamuzi watakayoyafanya yanapaswa kuakisi walichokipata kupitia kozi hiyo mara baada ya viongozi hao kurudi kwenye maeneo yao ya utendaji.
 
Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Agosti 2, 2022) alipofungua kozi fupi ya 13 ya viongozi katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Dar Es Salaam. Pia kozi hiyo itawaongezea uelewa na ufanisi katika eneo zima la ulinzi na stratejia kwa ajili ya kulinda maslahi mapana ya Taifa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
 
Waziri Mkuu amesema Serikali inatarajia kwamba washiriki wote, watatumia kikamilifu fursa hiyo adhimu kushiriki kwa umakini na uhodari wa hali ya juu ili kuongeza uelewa wao wa masuala mtambuka hususan ya kiulinzi, kiusalama na kistratejia.
 
Kozi hiyo inahudhuriwa na baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Maafisa Waandamizi kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Taasisi za Kimkakati za Serikali.
 
“Sisi viongozi wenu tunatarajia kuona kuwa mtakapohitimu mafunzo haya mtakuwa mmebadilika kimtazamo na hilo halinabudi kujidhihirisha kwa Wizara na Taasisi mnazotoka kuzungumza lugha moja katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi yetu.”
 
“Kwa kufanya hivyo, mtasaidia sana kusukuma maendeleo ya nchi yetu kwa haraka hasa katika kipindi hiki ambapo Serikali inalenga kukuza uchumi wa viwanda. Sambamba na hilo, tunapaswa kutambua kwamba changamoto za sasa ni mtambuka na si rahisi kutatuliwa na Wizara au Taasisi moja moja.”
 
Akizungumzia Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa chuo hicho uhakikishe  kozi hiyo inakuwa endelevu ili viongozi wengi zaidi wapite hapo na kufunzwa masuala muhimu yanayohusu ulinzi na usalama kwa nchi yetu.
 
“Tunahitaji viongozi, watendaji wakuu na maafisa waandamizi kutoka vyombo vya ulinzi na usalama na ofisi za kimkakati watambue na kuzingatia maslahi ya nchi, uzalendo, tunu zetu na nidhamu ya kazi kwenye utendeji wao.”
 
Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Meja Jenerali Ibrahim Mhona amesema chuo hicho tangu kianzishwe Septemba 2012 kimepata mafanikio mbalimbali ikiwemo kutoa kozi ndefu 10 pamoja na kozi fupi 12.
  
Mkuu huyo wa chuo ameongeza kuwa mafanikio mengine yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwake ni pamoja na kujitangaza na kukubalika kimataifa ambapo viongozi kutoka mataifa 16 wamehudhuria kozi mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo.
  
Naye, Kansela wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Balozi Dkt. Marten Lumbanga amesema mafunzo hayo yanayotolewa kwa viongozi yataleta matokeo chanya kwa washiriki na kulifanya Taifa lisonge mbele na salama kwani wataongezewa ueleewa na umakini katika usimamizi madhubuti wa sera kwa usalama wa nchi.

Posted by MROKI On Tuesday, August 02, 2022 No comments

July 30, 2022

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Melia Mkoa wa Kaskazini Unguja Zanzibar tarehe 30 Julia, 2022

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 Mhe. Anne Makinda akizungumza wakati wa kikao hicho.

Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakirishi) Mhe. Hamza Hassan Juma  akizugumza  wakati wa kikao hicho.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Kaspar Mmuya akizungumza wakati wa kikao hicho.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Dkt. Mhe. Jenista Mhagama akichangia hoja wakati wa kikao hicho.

Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia hoja wakati wa kikao.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa pamoja na Mtakwimu Mkuu Zanzibar Bw. Salum Kassim Ali wakifuatilia kikao hicho.
Posted by MROKI On Saturday, July 30, 2022 No comments

October 10, 2019


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa, Olman Ndetembea ambaye ni Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tekinolojia cha Mbeya na Mbunifu kiti maalum cha walemavu ambacho pia kinaweza kutumiwa kama kitanda au kifaa cha mazoezi ya kusimama katika maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mpilipili mjini Lindi, Oktoba 10, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuui, Sera, Bunge, Ajira, Vijana, Kazi na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (wa pili kulia) wakizungumza na vijana wa Kikundi cha Kimataifa cha Vijana (International Youth Felloship – IYF) wakati alipotembelea banda la kikundi hicho katika maonyesho ya wiki ya Vijana Kitaifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mpilipili mjini Lindi, Oktoba 10, 2019.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chupa yenye dawa za kulevya wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya wakati alipofungua maadhimisho ya wiki ya Vijana Kitaifa kwenye Viwanja vya Mpilipili mjini Lindi, Oktoba 10, 2019. Kushoto ni Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana, Kazi na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Wapili kulia ni Kamishina wa Kinga na Tiba wa Mamlaka hiyo, Peter Mfisi.

Vijana wa Lindi wakiandamana mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozindua Maadhimisho ya wiki ya Vijana kitaifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya mpilipili mjini Lindi, Oktoba, 10, 2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua maadhimisho wiki ya Vijana kitaifa kwenye viwanja vya Mpilipili mjini Lindi, Oktoba10, 2019.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza watendaji katika ngazi zote wahakikishe kuwa vijana wanawezeshwa kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Oktoba 10, 2019) wakati akizindua maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa mwaka 2019 kwenye viwanja vya Mpilipili, nje kidogo ya mji wa Lindi.

“Vijana tushirikiane na Serikali na kufanya kazi kwa bidii ili kuunga mkono jitihada za Serikali yetu ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwaletea wananchi maendeleo. Hatua hii itatuwezesha kama Taifa tuvuke na tufikie uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025,” amesema. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

Posted by MROKI On Thursday, October 10, 2019 No comments
  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo