Nafasi Ya Matangazo

April 07, 2012

''Hata tukiwa na uwezo wa kuhamisha milima kama hatupendani ktk tasnia ni kazi bure,kile kilicho moyoni ndio kioneshe usoni na sivinginevyo kama wanichukia moyoni basi onesha usoni na kama wanipenda moyoni basi onesha usoni na si vinginevyo,Isiwe moyoni wanichukia alafu usoni wanichekea,Hii sanaa ni karama tuliyobarikiwa na Mungu tuitumie vyema kwa ajili ya utukufu wake maana ipo siku atatuuliza na kutudai,kama katupa bure basi anao uwezo wa kutuny'ang'anya pia'' soma Wakorintho uone jinsi Mungu alivyogawa karama hizi na ni kwanini katugawia.

Haya si maneno yangu bali ni yake Marehemu Steven Kanumba ambayo aliyasema wakati wa Tuzo za ZIFF kule Zanzibar.

Bila shaka hii leo wakati tunaenda Kupokea Ufufuo wa Bawana wetu Yesu Kristo hiyo kesho (Pasaka) Kanumba kama atapata nafasi ya kuhojiwa huko aliko hii leo juu ya Karama ya uimbaji na uigizaji aliyopewa aliitumia vipi basi jibu Alisha tuachia na hakika usoni alituonesha dhahiri kuwa uigizaji anauweza na kipaji anacho sijui katika matendo yake ya kumpendeza Mungu moyoni.

Wengi wamekufa, katika tasnia ya Filamu na maigizo hapa nchini, lakini kifo cha Steven Kanumba "The Great Pioneer" kinasemwa kuwa ni kifo kilicho leta kishindo na mshtuko mkubwa sana miongoni mwa wasanii na wapenzi wa filamu hapa nchini.

Mitandao mingi ya kijamii imetapakaa habari mbalimbali juu ya Kifo cha Msanii wa Magizo na filamu nchini Tanzania, Steven Kanumba.

Steven Charles Kanumba (28) ndio jina lakehalisi akiwa ni mtoto pekee wa kiume katika familia ya Bwana na Bibi, Charles Meshak Kanumba.
Kanumba alizaliwa yeye na dada zake wa wili huku yeye akiwa ni mtoto wa mwisho katika familia hiyo.
Alizaliwa januari 8, 1984, akiwa ni Msukuma kutoka mkoani Shinyanga alipata elimu yake ya Msingi katika shule ya Msingi Bugoyi mkoani humo.
Alipo maliza elimu yake ya Msingi Kanumba alijiunga na elimu ya Sekondari katika shule ya Mwadui seminari na baade alipofika kidato cha pili kuhamia katika Shule ya Christian a Seminari iliyopo jijini Dar es Salaam.
Alihitimu kidato cha sita katika shule ya Sekondari Jitegemee inayomilikiwa na Jeshi .
Kanumba aliwahi simulia kuwa uigizaji ni kitu ambacho kipo katika damu yake na alikuwa akikipenda na kutamani kuwa mwigizaji tangu akiwa mdogo. Alianza uigizaji akiwa mdogo kwa kufanya maigizo Kanisani.

Mbali na Uigizaji Kanumba pia alipenda sana kuimba na alifanya hivyo akiwa kanisani na shuleni.

Baada ya kuambiwa na watu kuwa anakipaji cha kuigiza ndipo Marehemu Kanumba alipoamua kujiunga na kundi la Kaole ambalo lilikuwa na waigizaji wakongwe ambao hivi sasa baadhi yao wamefariki kama akina mzee Kipara, Pwagu na wengine waliopo kama akina Bui Mwenda, Mashaka na wengine wengi.

Kanumba akiwa katika kundi hilo mbali  ya kukutana na wasanii hao wakomngwe ambao alijifunza mengi lakini pia alipata kufundishwa akiwa hapo na walimu kadhaa kutoka chuo cha Sanaa Bagamoyo.

Kanumba baada ya kukaa kwa takribani mwaka mmjoa akijinoa na Kaole sanaa Group alipata mafunzo pia ya uigizaji kutoka Chuo Kikuu cha  Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Dkt Nyoni ambaye alimfunza kwa miezi 3.

Hakika ni kipaji chake cha uigizaji mahiri na kuipenda kazi yake ndivyo viliweza kumjengea jina marehemu Kanumba na hatimaye kuweza kuanza kuteka hisia za watu na mashabiki.

Kanumba alijizolea Sifa nyingi sana ambazo kwa kiasi kikubwa zimemletea mafanikio katika tasnia ya filamu hapa nchini.

Kanumba baada ya mafanikio hayo katika uigizaji alimua kupiga hatua mbele na kuingia katika ulingo wa utengezaji wa filamu hapa nchini.

Katika filamu napo Kanumba amefanya fyema na kutamba vilivyo katika ualimwengu huu wa Filamu za Bongo “ Bongo Movie” na kulishika vilivyo soko hilo la filamu hapa nchini.

Kanumba aambaye ametutoka ghafla kwa maana ya bila kuugua na kifo chake kustua wengi hasa katika mapenzi yao makubwa katika filamu zake wataendelea kumkumbuka katika filamu zake kali za kusismua na mafunzo lukuki za Kiswahili.

Miongoni na Big Dady, Because of You, Devel Kingdom, Moses, This is It, More Than Pain, Off Side, Uncle JJ, The Shock, Young Billionaire na Description filamu iliyopo sokoni hivi sasa ni Kijiji cha Tambua HAKI na hivi karibuni alikuwa njiani kuzindua filamu yake mpya ya Ndoa Yangu.

Ni filamu ambazo hizi ambazo ziliweza kumzungusha Kanumba katika nchi mbalimbali duniani kama Nigeria, Ghana, Amerika na ulaya katika ama kurekodi filamu hizo au kukutana na watu mbalimbali wa tasnia yake na kujifunza mengi.

Zipo Filamu kati ya hizi ambazo ameigiza na waigizaji kadhaa kutoka Nigeria na Ghana.

Kanumba alipata mwaliko wa kushiriki katika tamasha kubnwa la Filamu la Nchini Ghana ambalo linajulikana kamam Festival of Films in Africa (FOFA 2012) lililofanyika katika mji wa Accra Ghana.

Hapa nchini Kanumba atakumbukwa sana na wacheza filamu na wazalishaji kama yeye ambao katika uhai wake aliwahi kufanya nao kazi kama vile Pitchou Mwamba, Ray, Aunt Ezekiel, JB, Wolper, Irine Uwoya, Aunt Ezekiel, Lulu, Jenifer,  Patrick, Sofia, Rich Rich, na wengineo kibao.

Nje yamipaka ya Tanzania kanumba amewahi kuigiza filamu zake hizo na wasanii Nollywood kule  Nigeria na alipata pia kutembelea ngome ya Hollywood, Warner Bros Pictures, Universal Studios na Disney Land.

Kanumba pia amep[ata kushinda tuzo mbalimbali kama vile Best actor  ya ZIFF, BEST FILM IN SOUND(DEVIL KINGDOM) aliyecheza na Mwigizaji Nguli wa Nigeria Ramsey.
Kanumba katika vitu ambavyo aliwahi kuvitamka kuwa anavipenda ni watoto nadhani ndio maana hata katika moja ya filamu zake aliigiza na watoto tu Jeniffer na Patriki katika Filamu ya Uncle JJ na hivi karibuni aliongeza mtoto mwingine machachari Sofia.

Pia alipenda kujichanganya na marafiki na kuwa na mitoko kiasi na kupebnda sana kuangalia filamu.
Posted by MROKI On Saturday, April 07, 2012 10 comments

10 comments:

  1. cjui kama mnayoyasema watanzania yanatoka uvunguni mwa mwa nyoyo zenu, kanumba amefanya uchafu mwingi iweje leo mseme alale mahali pema peponi?????????????

    ReplyDelete
  2. HAMNA CHA KUREXT IN PC HAPA ACHAWAFCKA TZ WAPUNGUE KUNA WENGINE WAMEBAK NABADO KUNA WA2 WANAISHI DUNIANI UTADHAN WANA HAT MILIKI YA KUISHI DUNIA TUNAPTA XO 2LOBAKIA JPANGE XAWAXAWA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1

    ReplyDelete
  3. nyie ndo washenzi kweli hamna utu,who are to judge others? wewe ndio una hati miliki,muacheni Kanumba arest in peace.

    ReplyDelete
  4. UKWELI NIKWAMBA TUSIANGALIE FLANI KAFANYA NINI BALI TTUIGE MAZURI MABAYA TUYAACHE KWANI HAKUNA BINADAM ALIYE MKAMILIFU KWA KILA KITU. AFU WASANII MLIOBAKI MJITAHII KUWA WABUNIFU KATIKA MOVIE ZENU IL KUMUUENZI VIZURI MR. KANUMBA

    ReplyDelete
  5. Ndugu hakuna binadamu asiye na mabaya kwani hatujakamilika lakini kumbuka mema yake machache ndiyo tunayoyakumbuka na siyo mabaya....Pia sisi binadamu hatuna mamlaka juu ya mbingu an pepo kazi yetu ni kuwaombea marehemu anayejua wapi pakuweka roho zao ni mwenyezi mungu peke yake....

    ReplyDelete
  6. Kaka tulikupenda sana na pia 2na tambua kwamba wewe ndio msanii wa kwanza kutoka tzee kuigiza na top actors & actress P.I.P!

    ReplyDelete
  7. Revelation 22:15 says "Outside are the dogs, those who practice magic arts, the sexually immoral, the murderers, the idolaters and everyone who loves and practices falsehood". looks careful at the last words, God is caution us that whoever love and practice falsehood will go to HELL. Here, the Bible, is talking about acting and watching movies. Mr Kanumba died as an actor, then you can understand were he goes. As human beings we morn about him but entering paradise depends with you good deeds and acts before Jesus Christ, who is the only way to heaven.

    ReplyDelete
  8. jamani msimuhukumu the great, kwanza dada zenu walikuwa wakijipeleka wenyewe...jamaa alikuwa 'mwanaume' na hata huyo dogo mwenyewe kwa mwanaume yeyote aliyekamilika ni vigumu kumwepuka kwa jinsi alivyo....angalieni picha aliyopiga akiwa amelala huku amebinua kiuno chake kilichochorwa tattoo kama alivyofanya brandy wa marekani ktk moja ya picha zake (ingia google), nani angeweza kusema 'nguruwe pita sina nchale'?

    ReplyDelete
  9. There is a lot of ignorant comments in here, unbeliavable! So apparently, now actors are entittled to go to hell, I wonder what kind of a bibble some of us are reading. And who are you to judge Kanumba, I think we should leave that to God. And for you my friend, I would advise you not to occupy yourself with judging people because you might as well end up in hell for that.

    ReplyDelete
  10. ninachoweza kusema ni anaemhukumu marehemu huyo hajui anapotoka na hajui aendapo!mwenyezi mungu awasamehe 7bu hamjui mlitendalo!!

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo