Nafasi Ya Matangazo
Showing posts with label BUNGE. Show all posts
Showing posts with label BUNGE. Show all posts

January 31, 2024

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na  Mbunge wa Jimbo la Ismani William Lukuvi,  Bungeni jijini Dodoma, Januari 31, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na  Waziri wa Chi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama,  Bungeni jijini Dodoma, Januari 31, 2024. 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Det. Doto Biteko akiwasikiliza Waziri wa Chi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene na Mbunge wa Jimbo la Ismani William Lukuvi,  Bungeni jijini Dodoma, Januari 31, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Posted by MROKI On Wednesday, January 31, 2024 No comments
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akijibu swali la Mbunge wa Muleba Kusini, Mhe. Dkt. Oscar Kikoyo, kuhusu Sheria ya Bima na swali la Mbunge wa Konde, Mhe. Mohamed Said Issa kuhusu mkakati wa Serikali wa kuongeza mapato ya biashara zinazofanyika kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, bungeni Jijini Dodoma.
***********
Na  Khadija Ibrahim, WF, Dodoma
Serikali imewataka wananchi kutunza kumbukumbu na nyaraka muhimu za rejea ili kuondoa usumbufu na kurahisisha zoezi la ulipaji fidia hususan kwa wasimamizi wa mirathi kupitia bima walizokata.
 
Wito huo umetolewa bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati akijibu swali la Mbunge wa Muleba Kusini, Mhe. Dkt. Oscar Kikoyo, aliyetaka kufahamu wakati ambao Serikali itarekebisha Sheria ya Bima ya Tanzania ili kuweka kima cha chini cha malipo ya fidia kwa waathirika wa ajali za barabarani.
 
Alisema kuwa Septemba 2022, Mamlaka ya Bima Tanzania ilitoa Mwongozo unaotambulika kama Mwongozo wa Viwango Elekezi vya Fidia ya Bima kwa Madai ya Majeraha ya Mwili na Vifo kwa Mtu wa Tatu Kutokana na Ajali za Vyombo vya Moto.
 
“Mwongozo huo wa Viwango vya Fidia ya Bima ulitolewa kwa mujibu wa Kifungu cha 6 na 11 cha Sheria ya Bima Sura Na. 394, lengo likiwa ni kuweka usawa na ubora katika ulipaji fidia zitokanazo na madai ya bima”, alisema Dkt. Nchemba.
 
Alisema kuwa utekelezaji wa mwongozo huo umepunguza kwa sehemu kubwa malalamiko kutoka kwa waathirika wa ajali za vyombo vya moto kwa kuwa kuna usawa katika suala la viwango vya fidia vinavyotolewa na kampuni za bima.
 
Aidha alieleza kuwa Serikali itaendelea na jitihada za kujenga uelewa kwa wadau wa tasnia ya bima na wananchi kwa ujumla ili kutimiza matakwa ya Sheria ya Bima, Sura 394, ikiwemo kuboresha huduma za bima na kumlinda mteja.
 
Kwa upande mwingine, akijibu swali la Mbunge wa Konde, Mhe. Mohamed Said Issa kuhusu mkakati wa Serikali wa kuongeza mapato ya biashara zinazofanyika kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, Dkt. Nchemba alisema kuwa Serikali za pande mbili zimeendelea kuboresha na kutekeleza mikakati mbalimbali kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu mbalimbali za uwekezaji na biashara.
 
Alieleza kuwa baadhi ya mikakati iliyotekelezwa ni pamoja na kuboresha na kuunganisha mifumo ya kodi ya EFDMS na VFMS ili kusomana na kurahisisha utozaji kodi, ada na tozo, kuboresha mifumo ya urejeshaji wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na kurahisisha mifumo ya utoaji vibali, leseni na ukaguzi wa mizigo.
 
Aidha Mhe. Dkt. Nchemba alibainisha kuwa katika kuongeza uwazi, Serikali kupitia Mamlaka za Usimamizi wa Mapato zimeweka bango linaloonesha bidhaa ambazo hazipaswi kulipiwa ushuru au kodi na bidhaa zinazopaswa kulipiwa, pamoja na viwango vinavyopaswa kulipwa.
 
Alisema kuwa pande zote zimekubaliana kuwa ushuru wa forodha unaokusanywa kwa upande wa Zanzibar, uwasilishwe kwenye mfumo wa Hazina wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ili kuongeza tija katika ukusanyaji wa mapato na ufanisi katika udhibiti wa biashara za magendo.
Posted by MROKI On Wednesday, January 31, 2024 No comments
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akijibu maswali bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika Kikao cha pili Mkutano wa 14 wa Bunge jijini Dodoma leo Januari 31, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akijadiliana jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni katika Kikao cha pili Mkutano wa 14 wa Bunge jijini Dodoma leo Januari 31, 2024.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akijibu maswali bungeni jijini Dodoma leo Januari 31, 2024 kuhusu mkakati wa Serikali wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi, katika Kikao cha pili Mkutano wa 14 wa Bunge.
************
Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wizara za kisekta imeanza kufanya tathmini nchi nzima kubainisha maeneo yanayohitaji kufanyiwa maboresho kukabiliana na athari za kimazingira.
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtambwe Mhe. Khalifa Mohammed Issa aliyetaka kujua lini Serikali itafanya utafiti kuyabaini maeneo yaliyoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.
 
Katika kushughulikia changamoto ya mabadiliko ya tabianchi Dkt. Jafo amesema kuwa Serikali imeanza kuyafanyia kazi maeneo hayo kwa kutekeleza miradi ya mazingira pande zote mbili za Muungano.
 
Amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais inaendelea na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa tuta linalozuia maji ya bahari kuingia kwenye makazi na mashamba unaotekelezwa eneo la eneo la Sipwese Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini, Pemba.
 
Halikadhalika, amesema mradi huo unatekelezwa pia katika eneo la Mikindani, Mtwara ambako kunajengwa ukuta utakaosaidia kupunguza kasi ya maji ya bahari kuingia kwenye makazi ya watu na kuta kwa ajili ya kurejesha fukwe katika hali yake.
 
“Katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imetuma timu ya wataalamu ikishirikiana na wizara za kisekta kufanya tathmini ambayo itatusaidia kubaini maeneo gani yenye changamoto na kuyafanyia kazi hivyo kuhakikisha nchi yetu inakuwa salama,” amesisitiza Waziri Dkt. Jafo.
 
Awali, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis alisema Serikali inaendelea na kampeni za kuhamasisha wananchi kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo zoezi la upandaji wa miti katika maeneo yote nchini.
 
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Mariam Nasoro Kisangi aliyeuliza mkakati ya Serikali wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi, Mhe. Khamis alisema Ofisi ya Makamu wa Rais inafanya kampeni hizo kwa kushirikiana na taasisi kuhamasisha ubunifu, utafiti na uendelezaji wa teknolojia za kukabiliana na changamoto hiyo.
 
Mhe. Khamis alibainisha kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeandaa na kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (2021-2026) na Mpango Kabambe wa Taifa wa Hifadhi ya Mazingira (2022-2032).
 
Aidha, alisema kuwa kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar upo Mkakati wa Mabadiliko ya Tabianchi Zanzibar (2014-2030) ambao unatekelezwa kupitia Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais yenye dhamani ya mazingira.
 
Alisema Serikali inayo Mipango ambayo kwa pamoja imeelezea changamoto na hatua mbalimbali za kuzifuata katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi yanayoathiri maeneo mbalimbali hapa nchini.
 
“Tunatambua mkakati tulionao wa kusafisha mito na tayari Mhesehimiwa Waziri (Dkt. Jafo) alishaunda Kamati na kubaini chanzo mkusanyiko wa mchanga mkoani Dar es Salaam na kuziba mifereji nasi tunaendelea kutoa elimu na kusimamia Sheria ya Mita 60 na Usafishaji wa mito kwa kutoa mchanga na takataka nyingine,” alisema Mhe. Khamis.

Posted by MROKI On Wednesday, January 31, 2024 No comments

January 30, 2024

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akijibu swali la Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina, kuhusu kiasi cha fedha ambacho Serikali imewalipa wazabuni na wakandarasi wa ndani baada ya kuwasilisha madai yao na kufanyiwa uhakiki, bungeni Jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (kulia), bungeni Jijini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano, WF, Dodoma)
*************
Na. Khadija Ibrahim, WF, Dodoma
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameliambia Bunge, Mjini Dodoma kuwa katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2016/2017 hadi Desemba 2023, imewalipa wazabuni na wakandarasi wa ndani zaidi ya shilingi trilioni 2.1 kati ya madai ya zaidi ya shilingi trilioni 3.1 yaliyowasilishwa.
 
Dkt. Nchemba amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina, aliyetaka kufahamu kiasi cha fedha ambacho Serikali imewalipa ama kukataa kuwalipa wazabuni na wakandarasi wa ndani baada ya kuwasilisha madai yao na kufanyiwa uhakiki.
 
“Jumla ya madeni ya wazabuni na wakandarasi yaliyowasilishwa kwa uhakiki yalikuwa zaidi ya sh. bilioni 3,110.33kati ya kiasi hicho madeni yaliyolipwa ni zaidi ya sh. bilioni 2,128.54 ambapo sh. bilioni 1,032.13 ni madeni ya wazabuni na sh. bilioni 1,096.41 ni madeni ya wakandarasi” alisema Dkt. Nchemba
 
Alisema kuwa madeni ya sh. bilioni 981.79 yalikataliwa kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo kukosekana kwa nyaraka, madeni kubainika kulipwa tayari, pamoja na makosa ya ukokotoaji. 
 
Mhe. Dkt. Nchemba aliongeza kuwa Serikali kwa kutambua umuhimu na mchango wa Sekta Binafsi katika maendeleo na uchumi wa Taifa, imeendelea kutenga na kulipa madeni ya wazabuni na wakandarasi yaliyohakikiwa na kukubaliwa.
 
Alifafanua kuwa Serikali imeongeza bajeti ya kulipa madeni kutoka wastani wa shilingi bilioni 400 hadi shilingi bilioni 700 kwa mwaka na kuahidi kuwa  madai ya wazabuni na wakandarasi yataendelea kulipwa kadri watakavyowasilisha hati zao za kukamilisha kazi (certificates).

Posted by MROKI On Tuesday, January 30, 2024 No comments
  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo