Nafasi Ya Matangazo

March 01, 2016

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akipongezana na Meneja Mkuu wa Fastjet Tanzania, John Corse (kushoto) baada ya Airtel na Fastjet kuingia ubia wa kibiashara utakaowawezesha  Wateja wa Fastjet kununua tiketi za usafiri kupitia Airtel Money. Katikati ni Meneja wa Airtel Money, Asupya Naligingwa ambapo hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika leo katika ofisi za Airtel makao makuu Morocco jijini Dar es Salaam
************
Kampuni ya ndege ya ki-Afrika yenye gharama nafuu Fastjet, imekuwa ya kwanza kuingia kwenye makubaliano na kampuni ya simu ya Airtel Tanzania ambapo wateja wa Fastjet wataanza kununua tiketi na hata kufanya miamala mingine kupitia Airtel Money.

Kutokana na makubaliano hayo, wateja wa fastjet watakaoununua tiketi kupitia Airtel Money, watapata nafasi ya kushinda tiketi ya kusafiri wa ndani na nje ya nchi kupitia droo ambayo itafanywa kwa miezi miwili.

Akitangaza kusainiwa kwa makubaliano hayo, Meneja Mkuu wa Fastjet Tanzania, John Corse alisema: “ukweli kwamba wateja wetu watamudu kupata tiketi zao kupitia Airtel Money kunaimarisha kujituma kwetu katika  kuhakikisha kuwa Fastjet inaishi kulingana na ahadi yake ya kuwa shirika lisilo na usumbufu linalofanya safari za wateja wake kuwa ni rahisi.

Alisema kuwa huduma hiyo ambayo inampa mteja uhakika wa kupata tiketi za Fastjet kutoka mahali alipo kwa kutumia  simu za mkononi, itaanza Machi 03, 2016 na kuongeza kuwa mpango huo mpya wa kushirikiana na Airtel  sio tu kwamba utahakikisha kuwa huduma inakuwa ya kasi na ya ufanisi bali pia itaondoa kabisa kadhia ya kupoteza muda miongoni mwa wateja walipokuwa wanakwenda kununua tiketi kutoka kwa mawakala wa Fastjet waliopo mbali na makazi yao.

“Tunajivunia mno na tunawashukuru wateja wetu ambao wamekuwa wakituunga mkono na tunaahidi kuendelea kuwapa huduma zetu zenye ubora wa hali ya juu pamoja na kusikiliza mahitaji ya wateja wetu,” alisema Corse.

Akizungumza kuhusu makubaliano hayo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya alisema: “ushirikiano huu umekuwa ni njia sahihi kwa wateja wetu ya kulipia tiketi kwa safari zao za ndani na za kimataifa wakati wowote, mahali popote kwa utulivu wakiwa majumbani kwa kutumia  simu ya mkononi.

 “Tunaamini wateja wetu wa Airtel Money  kote nchini  hivi sasa watafurahia  njia hii ya haraka na rahisi kulipia  na hali kadhalika  kupanga safari zao na Fastjet katika mazingira ya utulivu.”

Aliongeza kusema, “Airtel itaendelea kuonesha  kujituma kwake katika kutoa bidhaa na huduma zilizojikita kwenye ubunifu, kuanzisha ushirikiano ambao ni muhimu na utakaokidhi mahitaji ya wateja kupitia huduma za Airtel Money  wakati wowote.”

Akiongelea promosheni hiyo, Meneja wa Airtel Money, Asupya Naligingwa alisema, “tutakuwa tunatoa zawadi kwa wateja watakaonunua tiketi za fastjet kupitia Airtel Money kila baada ya wiki mbili kwa miezi miwili. Tiketi hizi zitatolewa kupitia droo ambapo kumi na sita zitakuwa za safari za ndani ya nchi na nne zitakuwa za safari za nje ya nchi. Tunawaomba wateja kununua tiketi kupitia Airtel Money ili wapate nafasi ya kushinda tiketi za safari wazipendazo”, alisema Nalingiwa.

Nalingiwa alibainisha: “Ili kulipia tiketi, mteja anatakiwa kupiga: *150*60*#, halafu chagua, ‘lipia bili’, halafu, ‘chagua kwenye orodha’, halafu chagua, ‘Usafiri wa anga’, kisha ufuate maagizo”.
Posted by MROKI On Tuesday, March 01, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo