Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Dennis Londo, amewataka wafanyabiashara wa Tanzania kutumia fursa kubwa kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Soko Huru la Afrika, kuuza bidhaa zao.
Mhe. Londo ameyasema hayo wakati alipokuwa akifunga hafla ya utoaji tuzo za jukwaa la 4 la biashara na uwekezaji kwa Watendaji Wakuu na Wakurugenzi wa makampuni 200 ambalo linawakutanisha wadau kujadili namna ya kufungua fursa kwa watanzania, wajasiriamali kufanya biashara nje ya Tanzania.
Mhe Londo amesema kuwa uwepo wa jukwaa hili kunasaidia kuwakutanisha Wakurugenzi Makampuni kubadilishana uzoefu ma kuchangamkia fursa zilizopo.
Aliongeza kuwa Tanzania ni mwanachama wa EAC na SADC na sasa inaelekea kwenye Itifaki ya Soko Huru la Afrika, hivyo maandalizi ni sehemu muhimu ya kuhakikisha Watanzania wanashiriki na kunufaika na jumuiya hizo.



.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)



0 comments:
Post a Comment