Chama cha siasa kinapaswa kuwa na mikakati madhubuti ya kuwafikia wananchi wake, kuzungumza masuala mbalimbali ya maendeleo, kujadili changamoto zao na namna bora ya kuzitatua.
Katika ulimwenguni huu wa maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia, suala la matumizi ya vifaa vya kisasa vya mawasiliano hayana budi kutumika.
Katika shughuli za Chama na mikutano ya hadhara, matumizi ya mziki hayaepukiki katika kuhakikisha hadhira yote inasikia kinachozongumzwa katika meza kuu au jukwaani.
Hivyo basi, katika kuhakikisha shughuli na mikutano ya hadhara inawafikia wananchi wengi zaidi, Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Tanga, kimenunua mziki mkubwa na wa kisasa kufanikisha azma hiyo.
Mziki huo wenye vyombo vya kisasa, gari la matangazo na jenereta kubwa, vimenunuliwa na Mwenyekiti wa CCM mkoani humo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu (MCC), Rajab Abdallah, maarufu 'Ustadhi Rajab.'
Vyombo hivyo vya kisasa vinatarajiwa kutumika katika shughuli na mikutano mbalimbali ya Chama mkoani humo.
Ikumbukwe kuwa, CCM ina wajibu wa kuzungumza na wananchi juu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na mikakati mbalimbali ya maendeleo inayoratibiwa na serikali katika kuwahudumia wananchi katika kukuza maendeleo na ustawi wao.
Aidha, mziki huo pia, unatarajiwa kutumika katika kampeni mbalimbali za uchaguzi ili kuwafikia wananchi wengi zaidi waliopo katika viwanja na waliobaki nyumbani.
Kwa ukubwa wa mziki huo, waliopo viwanjani na waliobaki nyumbani, wote kwa pamoja watasikia ujumbe unaozungumzwa kutokana na vyombo hivyo kuwa vyenye uwezo mkubwa na vya kisasa zaidi.
Hakika, Mwenyekiti Rajab amefanya jambo kubwa kufanikisha ununuzi wa mziki huo ambao utasaidia kuwafikia wananchi wengi kwa wakati mmoja na hivyo kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa wananchi.
Muhimu ni vyombo hivyo kutunzwa na kuhifadhiwa vizuri, ili malengo ya ununuzi wake yatimie katika kuhakikisha vinasaidia katika ujenzi wa Chama na kuzungumza na wananchi.










0 comments:
Post a Comment