Nafasi Ya Matangazo

September 07, 2026

Mwenza wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Hafidh Ameir Hassan, amefariki dunia Septemba 7, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Deogratius Ndejembi, Hafidh Ameir Hassan amefariki wakati akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo Zanzibar.

Ndejembi amesema Mzee Hafidh amefikwa na umauti leo Saa mbili asubuhi akipatiwa matibabu katika Hospitlai ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena visiwani Zanzibar.

“kwa masikitiko makubwa, nawajulisha taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Hafidh Ameir Hassan, Mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kilichotokea leo tarehe saba Septemba 2026, majira ya saa mbili ya asubuhi, katika Hospitali ya kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo,”

“Ninatoa pole kwa Mheshimiwa Rais, familia, ndugu, jamaa na marafiki, na Watanzania wote kwa msiba huu, mpango wa mazishi unaendelea kufanyika Kizimkazi, Zanzibar,”

Marehemu Hafidh Amir Hassan na Rais Samia walifunga ndoa mwaka 1978 na kufanikiwa kupata watoto kadhaa akiwepo Naibu Waziri wa Elimu, Wanu Hafidh Amir. 

Aidha mipango ya mazishi inafanyika Kizimkazi Zanzibar nyumbani kwa marehemu ambapo taarifa zinaarifu kuwa maziko yanataraji kufanyika hii leo Septemba 7, 2026 Saa 10:00 alasiri. 

Posted by MROKI On Monday, September 07, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo