Nafasi Ya Matangazo

September 07, 2026

Waziri wa Ujenzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Abdallah Ulega amewaasa wanafunzi nchini kusoma kwa bidii, kuipenda nchi yao na kujituma ila kufikia malengo yao.

Ulega ameyasema hayo wakati akizungumza na wanafunzi hao kwa njia ya simu wakati wa uterkelezaji wa programu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke ya kuwakutanisha watu mashuhuri waliosoma katika shule za msingi na sekondari nchini.

Ulega aliwakilishwa na Mke wake ambaye ni Mbunge wa Viti maalum Pwani, Mhe. Mariam Ulega na kuzungumza na  walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Karibu ambayo zamani ilikua shule ya Msinhgi Muungano.

Akizungumza na hadhara hiyo kwa njia ya simu, Waziri Ulega amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke kwa kubuni program hiyo ambayo inatoa hamasa kwa wanafunzi kujibidisha katika masomo ili watimize ndoto zao kitaaluma.

Aidha ameishukuru Shule ya Msingi Muungano na sasa Karibuni Sekondari kwa kumjenga vyema huku akiwaasa wa wanafunzi wa shule ya Sekondari Karibuni kusoma kwa bidi ili kuwa watendaji bora.

“Lakini niseme tu kwa wanafunzi,   wafanye jitihada ya kusoma ili kuwa watenda kazi wema katika taifa na watambue kuwa nchi hii ni yao na waanze kujifunza kuwa na tabia njema,”alisema Ulega.

Ulega amesema wanafunzi wanapaswa kutambua kuwa nchi hii ina fursa kwa kila mmoja wao, bila kujali anatoka wapi katika kila pande ya nchi hii na kinachohitajika ni kujifunza kwa bidi, kuipenda nchi na kujituma.  
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Kungu John Malulu pamoja na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP. Emma Foya ndio walioongoza programu hiyo shuleni hapo.

Lengo la Programu hiyo inayotekelezwa nchi nzima  ni kushawishi wanafunzi kusoma kwa bidii ili wafikie malengo yao na kufikia malengo kama ya watangulizi wao au kuwazidi watu hao maarufu ambao walisoma katika shule zao.

Posted by MROKI On Monday, September 07, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo