Nafasi Ya Matangazo

September 18, 2026

Ni Sekunde, Dakika, Saa, Siku, Wiki, Mwezi, Mwaka na hatimaye mika 19 sasa imetimia tangu Mzee S. T Nathan (18/08/1925 – 18/09/2007) ututangulie Mbele za haki kama ulivyotutangulia kuja duniani.

Nimajonzi sana kwetu na pengo lako halijazibika hadi hivi leo.

Unakumbukwa na wengi sana maana ulikuwa ni mhimili mkuu katika familia, kipekee unakunbukwa na Mke wako, watoto wako wote, wakwe zako, wajukuu  na vitukuu.

Aidha, unakumbukwa na Ndugu zako, Wananchi na majirani zako wa pale Kijiji cha Kinyenze,Kata na Tarafa ya Mlali , Wilayani Mvomero mkoani Morogoro, Same na Ugweno mkoani Kilimanjaro pia wanakukumbuka sana na kukuombea kila lililo jema katika mapumziko yako.
 
Tunakumbuka maneno yako ya Mwisho uliyotuachia watoto wako kuwa TUPENDANE, TUSAIDIANE na TUSHIRIKIANE, baba hakika hili linatendeka na tupo na umoja uliotujengea na tunajivunia hilo daima.

Tunazidi kukuombea Baraka na pumziko jema maana sote uliotuacha tutakufuata kama tulivyo kufuata hapa duniani.
PUMZIKA KWA AMANI MZEE S.T NATHAN
Jina la Bwana Lihimidiwe Amina.
Posted by MROKI On Friday, September 18, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo