Taarifa hiyo inatokana na
agizo alilolitoa Mhe. Rais Samia tarehe 28 Machi 2021, wakati akipokea Taarifa
ya CAG kwa mwaka 2019/ 2020.
Katika taarifa ya ukaguzi
maalum, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bw. Charles Kichere amesema
katika ukaguzi uliofanyika imebainika kuwa fedha zilizotolewa BoT katika kipindi hicho zilifuata
taratibu zote, isipokuwa baadhi ya malipo yaliyokuwa yanatoka Hazina Kuu kwenda
katika Taasisi mbalimbali za Serikali yalibainika kuwa na mapungufu.
Mapungufu hayo ni pamoja na
baadhi ya taasisi kama vile Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na Mamlaka ya
Bandari Tanzania (TPA), kufanya malipo mara mbili kwa kazi moja au kuchelewa
kutumia fedha zilizoidhinishwa kwa ajili ya malipo ya kazi husika.
Vilevile, CAG Kichere amesema
yamejitokeza mapungufu ambapo baadhi ya Makandarasi waliotoa huduma
kucheleweshewa malipo yao hali inayosababisha madeni ya makandarasi kuwa makubwa
kutokana na riba ambayo ni mzigo kwa
Serikali.
Mapungufu mengine ni pamoja na
kuwepo kwa miradi ambayo haikupangwa na hivyo kufanya malipo nje ya bajeti ya
Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Taarifa ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi, inayotarajiwa kufanyika mwezi Agost,2022, kutoka kwa Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa, leo Julai 01,2021 Jijini Dodoma.
Dkt. Chuwa amesema Sensa ya
mwaka 2022 itatumia teknolojia ya kisasa ya Kidijitali chini ya mfumo ulipo wa
Serikali katika ngazi zote za Utawala kwa pande zote za Muungano.
Aidha, amesema Sensa ya majaribio itafanyika mwezi Agosti mwaka huu (2021) katika mikoa saba kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment