Nafasi Ya Matangazo

July 02, 2021

Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango akifanya mazungumzo na Shirikisho la Wafanya biashara wa Ufaransa (MEDEF)  Mjini Paris – Ufaransa. Shirikisho hilo linahusisha baadhi ya kampuni kubwa kama vile TOTAL ENERGIES na AIR BUS ambazo tayari zimefanya uwekezaji katika maeneo mbalimbali nchini.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango akifanya mazungumzo na Shirikisho la Wafanya biashara wa Ufaransa (MEDEF)  Mjini Paris – Ufaransa. Kulia ni RAis wa MEDEF,  Momar Nguer.

Mkutano huo ukiendelea


Makamu wa Rais amekutana na kufanya mazungumzo na shirikisho la wafanya biashara wa Ufaransa ( MEDEF) Paris – Nchini Ufaransa.

Mhe. Makamu wa Rais alitumia fursa ya mkutano huo kuzikaribisha Kampuni za Ufaransa kuja kuwekeza nchini Tanzania hususan katika sekta za kipaumbele kwa Serikali ya Awamu ya Sita ikiwemo ujenzi wa miundombinu, kilimo, elimu, afya na utalii.

Mheshimiwa Makamu wa Rais aliwahakikishia Wafanyabiashara hao kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan inachukua hatua mbalimbali kuboresha mazingira ya uwekezaji na ushirikishwaji wa sekta binafsi katika uchumi wa Tanzania na hivyo uwekezaji wao utakuwa katika mikono salama.

Mheshimiwa Makamu wa Rais aliwafahamisha wafanyabiashara hao baadhi ya jitihada zinazoendelea kufanywa na Serikali ili kuvutia wawekezaji ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya kisasa kama Reli ya Mwendokasi (Standard Gauge Railway), mradi wa umeme wa Julius Nyerere utakaozalisha megawati 2115, miradi ya maji na uboreshaji wa miundombinu ya barabara na usafiri wa anga.

Kwa upande wao, Kampuni hizo zilionesha kuridhishwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuahidi ushirikiano wa karibu katika utekelezaji wa miradi ya kipaumbele. Aidha, kama ishara ya kuunga mkono jitihada hizo, Kampuni hizi zilifahamisha kuwa zinatarajia kufanya ujumbe ziara nchini Tanzania kabla ya mwisho wa mwaka 2021 ili kuangalia fursa za uwekezaji.

Baadhi ya Kampuni kubwa za Ufaransa zilizoshiriki mazungumzo hayo ni pamoja na TOTAL ÉNERGIES na AIRBUS ambazo tayari zimefanya uwekezaji mkubwa nchini katika maeneo mbalimbali. 

Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika Picha ya pamoja na RAis wa shirikisho la wafanyabiashara wa Ufaransa (MEDEF)  Momar Nguer wakati walipokutana kufanya mazungumzo na shirikisho hilo Paris Nchini Ufaransa.



Posted by MROKI On Friday, July 02, 2021 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo