Wizara ya Kilimo kwa
kushirikiana na wadau inaendesha makongamano kuhusu mifumo ya chakula kwa lengo
la kukusanya maoni yatakayosaidia nchi
kuboresha mifumo ya chakula na
kuimarisha lishe ikiwa ni utekelezaji wa malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya
Umoja wa Mataifa (SDGs).
Akifungua kongamano la mifumo
ya chakula kwa wakulima, wafugaji,
wavuvi na wadau wengine wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini leo (01.07.2021) mjini Njombe kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara
ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Mkurugenzi Msaidizi Sera na Mipango Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Mbaraka Stambuli, alisema mikoa ya Njombe ,Songwe, Ruvuma na
Rukwa inaongoza kwa kuwa na watoto wenye udumavu .
Aliongeza kusema mikoa ya
Nyanda za Juu Kusini ndio inaongoza kwa kwa uzalishaji mkubwa wa chakula lakini
jambo la kushangaza ukanda huu ndio wenye hali duni ya za lishe.
Stambuli alisema kongamano la
mifumo ya chakula linalenga kujadili changamoto muhimu katika mifumo ya chakula
kwa kuzingatia ikolojia kwenye kanda ili kufanya dunia kuwa na uhakika wa
chakula na lishe bora.
“Kwa mfano mkoa wa Njombe
ndiyo wenye asilimia kubwa ya Watoto wenye udumavu (53.6%) amba[o mikoa mingine
yenye udumavu zaidi ya asilimia 40 ni Songwe (43.3%), Ruvuma (41.0%), Rukwa (
47.9 %) na Iringa (47.1%) ambapo takwimu hizi zinaashiria matatizo katika mfumo
wa chakula hivyo wadau wanatakiwa kutafuta majawabu kuboresha hali ua lishe
nchini “ alisema Stambuli.
Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu
Mifugo alibainisha kuwa mfumo wa chakula una mafungamano na changamoto ikiwemo
mabadiliko ya tabia nchi pia mwenendo mbaya wa hali ya hewa, magonjwa sugu, maonjwa
yasiyo ya kuambukiza na lishe duni ikiwemo athari za kutozingatiwa u salama na
ustawi wa wanyama.
Stambuli alibainisha kuwa Wizara
ya Kilimo imepewa jukumu la kuratibu na kuhakikisha wadau wote wa sekta ya umma
na binafsi katika mfumo wa chakula wanashiriki mijadala ambapo mapendekezo ya
nchi yatawalishwa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika mwezi
Septemba mwaka huu New York Marekani.
Akizungumza kuhusu lengo la
kongamano la mfumo ya chakula Mwakilishi toka Wizara ya Kilimo Magret Natai alisema
maana ya ‘ Mfumo wa Chakula ni mkusanyiko wa shughuli zinazohusiana na
uzalishaji ,usindikaji,usafirishaji ,uhifadhi na ulaji wa chakula ‘.
Natai alibainisha kuwa kupitia
kongamno hilo wadau watapata muda wa kujadiliana mifumo sahihi itakayoongeza
kasi ya namna dunia inavyozalisha, inavyotumia chakula na mtazamo wake kuhusu
chakula.
Wakizungumza kwenye kikao
hicho wawalikishi wa wakulima kutoka Njombe,Iringa,Mbeya ,Songwe na Ruvuma wakiwemo Benno Mgaya kutoka SAGCOT Songea
alisema ili kukabiliana na changamoto za udumavu elimu kwa shule za msingi na
sekondari ni muhimu ikiwemo suala la lishe bora.
“Ni muhimu shule zote nchini
ziwe na bustani za mboga mboga na matunda ili kuwajengea watoto uelewa wa
umuhimu wa lishe bora wakiwa bado wadogo” alisisitiza Mgaya
Naye Martin Haule mfugaji
kutoka wilaya ya Njombe alisema Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni
alisisitiza suala la lishe bora ili kuepukana na hali ya udumavu ambapo amewataka wazazi kutoa chakula bora na
kwa wakati kwa watoto wao .
Haule alibainisha kuwa kwa
Njombe tatizo la udumavu linachangiwa na “ wazazi kwenda mashambani na kurudi
jioni hivyo watoto wanashinda na njaa au watoto wanapewa ulanzi na komoni
badala ya chakula bora hivyo udumavu kuendelea” alisema.
Majadiliano kuhusu mifumo ya
chakula yanafanyika nchini kwenye kanda mbalimbali chini ya uratibu wa
Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula Dkt. Honest Kessy (Country Converner) aliyeteuliwa kuratibu
mijadala hii kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Andrew Massawe.
Kongamano la Mifumo ya Chakula Nyanda za Juu Kusini Njombe linafanyika sambamba na jingine linalofanyika Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza ili kupata mapendekezo ya nchi na hatua za kuimarisha mifumo ya chakula yakihusisha wadau wa maendeleo wakiwemo AGRA, FAO, WFP, GAIN na SAGCOT.
0 comments:
Post a Comment