Nafasi Ya Matangazo

March 18, 2019

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai akizungumza wakati wa halfa ya uzinduzi wa ofisi za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) jijini Dodoma leo. Baada ya maboresho makubwa ndani ya shirika hilo ikiwa ni pamoja na ununuzi wa ndege mpya za kisasa na kuongeza wigo wa safari zake, ATCL imeamua kufungua ofisi zake jijini humo badala ya kuendelea kutumia mawakala pekee.
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amewataka wabunge, Maofisa wa Serikali, wafanyabiashara na wajasiriamali kutumia huduma za ATCL  popote zilipo ndani na nje ya nchi ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya kufufua na kulijengea uwezo shirika hilo.Akifungua ofisi ya ATCL mkoani hapa, Ndugai alisema Watanzania wote kwa ujumla wao wakiwemo wanatakiwa kutumia huduma za ndege hizo ili kuunga mkono jitihada za serikali katika kuinua usafiri wa shirika hilo ambalo asilimia 100 ni mali ya Tanzania.Alisema kwa kutumia usafiri  ATCL wa ndani na nje ya nchi na katika nchi mbalimbali inakofika, ni uzalendo ambao hata mashirika ya ndege ya nje yanafanya hivyo, isipokuwa inapokuwa kuna sababu maalumu zinazochangia kutotumia usafiri huo.Ndugai alitoa rai kwa mawakala 300 wa shirika hilo waliosambaa ndani na nje ya nchi, kuzitangaza huduma nzuri na bora za ATCL popote zinapotolewa na kuzionesha kwamba ni za ubora wa hali ya juu na za daraja la juu. 

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele akizungumza katika hafla hiyo na kuwataka watendaji wa shirika hilo kuendelea kupanua na kuboresha huduma za usafiri wa ndani na nje ili kushinda katika soko la usafiri wa anga katika maeneo hayo.Aliwatoa hofu Watanzania na akawataka waendelee kutumia huduma za ATCL kutokana na mkakati wa kutunza rekodi za usalama wa anga kwani huduma za shirika hizo ni za kiwango cha juu. Baadhi ya watumishi wa ATCL na wageni mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo wa ofisi za ATCL jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge Job Ndugai na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele wakichukua mkasi tayari kwa uzinduzi.
  Spika wa Bunge Job Ndugai na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele wakiwa tayari wamekata utepe kuzindua ofisi za ATCL jijini Dodoma.
Spika wa Bunge Job Ndugai (kushoto) akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele wakichukua mkasi tayari kwa uzinduzi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele akisalimiana na mmoja wa wahudumu wa ofisi hiyo ya ATCL jijini Dodoma. Kulia ni   Spika wa Bunge Job Ndugai.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Richard M. Mayongela akizungumzia huduma za ATCL katika viwanja mbalimbali nchini. 

 Mmiliki wa Kiwanda Mvinyo cha Alko Vintage cha jijini Dodoma, Archard Kato akionesha bidhaa za kiwanda chake ambazo zinapatikana katika Ndege za ATCL jambo ambalo linachangia ukuaji wa soko la zabibu jijini Dodoma. 
Posted by MROKI On Monday, March 18, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo