Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Majaji wa Mahakama
ya Rufani, Wenyeviti wa Bodi na kumpangia kituo cha kazi Balozi. Kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka
walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-
Jaji Latifa Alhinai Mansoor ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huu, Jaji Mansoor alikuwa Jaji Mfawidhi, Kituo Jumuishi, Morogoro;
Jaji George Mcheche Masaju
ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huu, Jaji Masaju
alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Mshauri wa Rais, Sheria;
Jaji Dkt. Deo John Nangela
ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huu, Jaji Dkt.
Nangela alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga;
Jaji Dkt. Ubena John Agatho
ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huu, Jaji Dkt. Agatho
alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Biashara, Dar es Salaam;
Balozi Dkt. Stephen John
Simbachawene amepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil. Balozi Dkt. Simbachawene
anachukua nafasi ya Balozi Prof. Adelardus Kilangi ambaye amepangiwa majukumu
mengine;
Bw. Uledi Abbas Mussa ameteuliwa
kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kipindi cha
pili; na
Prof. Zacharia Mabubu Mganilwa
ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara
(CBE). Prof. Mganilwa anachukua nafasi ya Prof. Wineaster Anderson ambaye
amemaliza muda wake.
Aidha, uapisho wa Majaji wa
Mahakama ya Rufani walioteuliwa utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.
Jaji Latifa Alhinai Mansoor ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huu, Jaji Mansoor alikuwa Jaji Mfawidhi, Kituo Jumuishi, Morogoro;
0 comments:
Post a Comment