Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa eneo hilo, Mhe. Ndejembi amesema baada ya kufanya vikao na mwekezani huyo, makubaliano yalifikiwa ya kuwapatia wananchi hao ekari 100 kwa ajili ya Makazi na matumizi mengine ambayo yatapangwa na Halmashauri
“Serikali hii ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inajali ustawi wa Wananchi wake na Wawekezaji. Tumefanya vikao na wenzetu wa Sisal Estate na tumekubaliana kwa pamoja zitolewe ekari 100 kwa wananchi. Hekari 70 zitatolewa kwa makazi ya wananchi na ekari 30 zitaenda kwa Halmashauri ili zipangiwe matumizi bora ya Ardhi" amesema Mhe. Ndejembi.
Aidha, Waziri Ndejembi ametoa wito kwa wananchi hao kuwa asijitokeze mwananchi mwingine kuvamia hilo na kuwataka kila mmoja awe mlinzi wa mwingine ili kuepusha migogoro mingine.
0 comments:
Post a Comment