Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagala akizungumza na mmoja wa wakulima aliowatembelea Wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala (kushoto) akiwa pamoja na Maafisa Kilimo wa Wilaya hiyo walipotembelea na kuzungumza na wakulima wa Pamba.
Shamba la pamba
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
IDADI ya wakulima wa zao la pamba Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma, wameongezeka kufuatia jitihada za Viongozi wa Wilaya hiyo kulifanya zao la pamba kuwa zao kubwa la biashara litakalo saidia Kupunguza umasikini kwa Wananchi.
Afisa Kilimo Wa Wilaya ya Kakonko ambaye pia ni Afisa wa zao hilo Daniel Tilia alisema wakulima wa pamba Wilayani humo wameongezeka kutoka Wakulima 247 kwa msimu wa mwaka 216/2017 kufikia Wakulima 1,306 kwa Mwaka 2017/2018 kutokana na Wakulima hao kuitikia wito wa serikali wa kufufua zao la pamba.
Alisema msimu uliopita Wakulima walikuwa wachache kutokana na Changamoto ya ukosekanaji wa pembejeo pamoja na Viuatilifu hali iliyopelekea idadi ya Wakulima kushuka kutoka 500 mwaka 2015/2016 hadi 247 waliolima hekta 141 na kupata tani 41 kutokana na changamoto hizo.
Halmashauri kwa kushirikiana na serikali wametatua Changamoto hizo ikiwa ni pamoja na kutoa mbegu na pembejeo kwa Wakulima 1306 na Waliolima hekali 2,840 na matarajio ya wilaya ni kupata tani 1159.61 kwa zao la pamba.
"Sisi kama serikali tumejipanga vizuri sana katika kuhakikisha zao hili linainua uchumi wa Wanakakonko, baada ya kuona changamoto zilizopelekea wakulima kupungua tuliandaa mpango wa kuwakopesha mbegu wakulima pamoja nanoembejeo mpaka sasa zoezi hilo limekamilika na tunatarajia kupata pamba ya kutosha, niwaombe wakulima kuendelea kulima Kitaalamu na kufuata maelekezo ya Wataalamu ilikuweza kufikia lengo", alisema Afisa kilimo.
Akizungumza mara baada ya ziara ya kutembelea mashamba ya Wakulima waliokwisha panda zao hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala alisema zao hilo Kwa Mkoa wa Kigoma linalimwa zaidi Wilayani Kakonko hivyo Mkoa kwa ujumla umeandaa mpango mkakati wa kuhakikisha zao hilo linalimwa kwa wingi; ikiwa ni pamoja na wananchi kupata viuatilifu kwa wakati na kuhakikisha pamba inalimwa kitaalamu na yenye tija.
Alisema Serikali imejipanga kuwawezesha wakulima wa pamba kupata soko lenye uhakika.
Aidha, wakulima wanatakiwa kulima kwa kufuata maelekezo kutoka kwa maafisa kilimo, wataalamu kuendelea kutembelea mashamba hayo ilikuweza kuwaelekeza wakulima namna ya kufanya na uangalizi wa pamba ili waweze kupata mazao ya kutosha na kupata faida.
Rabisoni Banga Yeye ni Mkulima na Mwezeshaji wa Wakulima wa Pamba katika kata ya Kanyonza wilayani Kakonko alisema pamba imekuwa mkombozi kwao kwani ndio zao lililokuwa likiwaingizia pesa nyingi lakini kwa Mwaka uliopita zao hilo wakulima wengi walishindwa kulima kutokana na wengi wao walipata hasara kutokana na mazao yao kuharibika kwa na Wadudu na upungufu wa Mvua, kwasasa serikali imetatua tatizo hilo na matokeo wameanza kuyaona.
Aidha aliwashauri Wakulima Wilayani humo waweze kulima pamba kwani pamba ni dhahabu nyeupe na inaweza kuwainua kiuchumi kwa haraka, na kwamba ni zao ambalo uuzaji wake hausumbui na endapo wakulima Wakijitokeza kwa wingi serikali itaendelea kuweka nguvu yake katika zao hilo na kuinua uchumi wa Wananchi wa Kakonko.
0 comments:
Post a Comment