Msanii Harmonize akiwa na Rafiki yake Sarah wakigawa chakula kwa Watoto wanaoishi katika Mazingira hatarishi ambao wanalelewa katika kituo cha Kulea Yatima cha EAGT Mtwara.
Msanii wa muziki wakizazi kipya Rajab Abdulkahal au Harmonize amekula chakula cha mchana na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi katika kituo cha kulelea Yatima cha Kanisa la EAGT mkoani Mtwara kama moja ya kuwapa matumaini katika Maisha ya kila Siku.
Harmonize akiongozana na rafiki yake wa kike anayejulikana kwa jina la Sarah amesema kuna watoto waliopoteza wazazi wao wakiwa na umri mdogo huku wakiwa na ndoto kubwa za kimaisha lakini zinaonekana kupotea kutokana hivyo wanahitaji kupewa moya na kuwa na bidii binafsi.
Hata Hivyo Msanii Harmonize amepata fursa ya kubadilishana Mawazo na watoto wenye Ndoto mbalimbali za kimisha na kuwasihi kumshirikisha Mungu kwa kila wanachokifanya.
Harmonize akiongea na Wandishi wa Habari Mara baada ya kumaliza Chakula cha Mchana alichokiandaa kwa ajili ya Watoto Yatima Mtwara.
0 comments:
Post a Comment