Nafasi Ya Matangazo

March 28, 2017

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akieleza umuhimu wa mfumo mpya wa Kielektroniki wa Kufuatilia Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu wakati wa uzinduzi wa mfumo huo Machi 28, 2017 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Dodoma na kulia kwake waliokaa ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiwasilisha hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mfumo wa Kielektroniki wa Kufuatilia Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Agustino Tendwa akiratibu shughuli ya uzinduzi wa mfumo wa Kielektroniki wa Kufuatilia Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu uliofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Machi 28, 2017.
Mchumi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Novatus Tesha akionesha namna mfumo wa Kielektroniki wa Ufatiliaji wa Taarifa za Serikali unavyofanya kazi kwa wajumbe wa mkutano huo (hawapo pichani) Dodoma.
Mchumi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Novatus Tesha akionesha namna mfumo wa Kielektroniki wa Ufatiliaji wa Taarifa za Serikali unavyofanya kazi kwa wajumbe wa mkutano wa uzinduzi wa mfumo huo Machi 28, 2017 Dodoma. 
*****************
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amezindua mfumo mpya wa Kielektroniki wa Kufuatilia Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu ulianzishwa kwa lengo la kusaidia upatikanaji na utoaji wa taarifa za utekelezaji kupitia mfumo wa kisasa (kidigitali).

Akizindua mfumo huo wakati wa mkutano na waandishi wa habari Machi 28, 2017 Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni, Waziri alieleza umuhimu wa mfumo huo kuwa  umejikita katika kusaidia Viongozi Wakuu kupata Taarifa za utekelezaji wa Maagizo yao na yale yaliyoelekezwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala.

“Mfumo huu utasaidia sana katika kufuatilia shughuli za Serikali ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa maazigo yote na ahadi zilizotolewa ili kuona utekelezaji wake kwa urahisi tofauti na ilivyokuwa awali” Alisema Mhe.Waziri.

Aidha mfumo utasaidia pia Ofisi ya Waziri Mkuu kuongeza ufanisi wa uratibu na ufuatiliaji wa shughuli za kila siku za Serikali kwakuwa taarifa zote zitapatikana kwa wakati na takwimu za uhakika.

Alibainisha kuwa, kuanzishwa kwa mfumo ni moja ya sehemu ya kuondoa changamoto kadhaa ikiwa ni kuongeza ufanisi maeneo yetu ya kazi “kuanzishwa kwa mfumo huo kutatua changamoto za uchelewashwaji wa taarifa, na kutowajibika kwa ujumla na kuleta ufanisi kazini”.Alisisitiza waziri.

Aidha kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Hamisi Mwinyimvua alibainisha kuwa mfumo umepitia hatua zote muhimu ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha Mawaziri wote, Makatibu Wakuu wote, Wasaidizi wa Mhe.Rais Jonh Magufuli na Watendaji  wa Serikali.

Kwa kumalizia Waziri alipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Wakala wa Serikali Mtandao kwa kuona umuhimu wa kuwepo kwa mfumo huu na kutoa rai kwa Watendaji wote wa Serikali kuutendea haki kwa kufanya kazi bila uzembe wowote. “rai yangu kwa Watumishi wa Umma wote Nchini kuwajibika kwa kufanya kazi kwani kupitia Mfumo huu, mzembe atajulikana na mchapa kazi atajulikana. Na ikumbukwe tu, wazembe na wavivu hawana nafasi katika Serikali ya Awamu ya Tano”.
Posted by MROKI On Tuesday, March 28, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo