Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Ukuzaji Ajira Godwin Mpelumbe akitoa mafunzo kwa wakulima na wasindikaji wa zao la nyanya na mchicha lishe juu ya namna ya kuongeza tija na ubora wa bidhaa wakati wa mafunzo yanaendelea mkoani Iringa 19 Januari 2026 (Picha na OWM-KAM)
Na OWM (KAM) - Iringa
Na OWM (KAM) - Iringa
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano imewanufaisha wakulima na wasindikaji wadogo 849 kupitia mafunzo ya ukuzaji ujuzi kwa wakulima na wasindikaji wadogo yanayolenga kuboresha mbinu za kilimo na kuongeza thamani katika uzalishaji wa mazao.
Akitoa mada kwenye mafunzo hayo namna ya kuongeza ujuzi kwa wakulima na wasindikaji wa zao la nyanya nachcha lishe leo (19 Januari 2026) mjini Iringa ,Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Ukuzaji Ajira Bw. Godwin Mpelumbe amewashukuru wakulima kwa kuitikia wito wa serikali kuhudhuria mafunzo hayo na akawasihi kutumia ujuzi walioupata kuwanufaisha wao na jamii .
“Nawashukuru sana wakulima wa maeneo haya maana tangu tuanze mafunzo haya tumewafikia watu 849 katika Mikoa ya Dodoma, Singida, Mbeya na Sasa tupo Iringa, nasisitiza ujuzi huu mtakao pata mkawe mabalozi kwa wenzenu na mkautumie ujuzi huu kwenye mashamba na biashara zenu ili ziweze kuongeza thamani ya mazao na kipato” alisema Mpelumbe.
Mpelumbe amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuwezesha upatikanaji fedha mafunzo kwa wakulima na wasindikaji ili kupata mbinu bora za shughuli hvyo kukuza kipato chao, ajira na wananchi kupata ujuzi unaowasaidia kwenye shughuli zao za kila siku.
Katika hatua nyengine mtaalam kutoka Taasisi ya Kilimo Tanzania (TARI) Emmanuel Mwenda amewafundisha wakulima namna Bora ya kupata mazao yenye tija, mbinu za kukabiliana na magonjwa haswa katika wakati huu wa mabadiliko ya tabia nchi pia amewafundisha namna ya kuongeza thamani katika mazao yao.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Sophia Dominick alisema wamefurahishwa na mafunzo waliyoyapata kwani wamejifunza kwa vitendo na nadharia ikiwemo kutembelea kiwandani na kujionea shughuli zinavyo fanyika na kubadilisha mitazamo walioyokuwa nayo kwa kupata elimu mpya ya kilimo biashara ambapo aliahidi kwa niaba ya wenzake kutumia elimu hiyo kuboresha uzalishaji na thamani ya zao nyanya na mchicha lishe.
Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Ajira na Mahusiano inaratibu programu ya ukuzaji Ajira kwa wakulima na wasindikaji nchini ili kuwajengea uwezo wa kuongeza tija na ubora wa bidhaa hatua itakayochochea kasi ya uzalishaji ajira na kuongeza kipato






0 comments:
Post a Comment