NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAIMU
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe amewataka
wananchi kuwa wavumilivu wakati Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),
likifanya jitihada za kufanya uchunguzi katika mfumo mzima wa Gridi ya
Taifa na kurekebisha hitilafu iliyopelekea kukosekana kwa umeme katika mikoa
yote iliyounganishwa na Gridi ya Taifa leo hii Machi 29, 2017.
Kwa
mujibu wa taarifa ya TANESCO kutoka kitengo cha Uhusiano Makao Makuu, imemnukuu
Profesa Mdoe, (pichani juu katikati) akiyasema hayo mbele ya Waandishi wa habari wakati wa ziara yake
ya kutembelea Mitambo ya umeme wa Gesi ya Kinyerezi I ili kufuatilia tatizo la kukatika
kwa umeme katika mikoa yote iliyounganishwa na Gridi ya Taifa saa 1:00 asubuhi
leo Machi 29, 2017.
Alisema
mara baada ya wataalam kutoka TANESCO kugundua hitilafu, walianza kushughulikia tatizo hilo na
kufanikisha kurejesha umeme katika mikoa ya Iringa ambayo ilipata umeme saa
1:27, Dar es Salaam saa 1: 43 pamoja na Zanzibar ambayo ilipata umeme saa 2: 42
na kuongeza kuwa ilipofika saa 6 mchana mikoa yote iliyounganishwa na Gridi ya
Taifa ilipata umeme kama kawaida.
Alieleza
kuwa uwashaji wa mitambo unaendelea na uchunguzi wa kubaini chanzo cha hitilafu
bado unaendelea.
Wakati
huo huo Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji (anayeshughulikia usafirishaji umeme), Mhandisi
Kahitwa Bishaija alisema mpaka sasa tatizo limeshadhibitiwa na kwamba
wanaendelea na uchunguzi chanzo cha tatizo hilo ili kudhibiti lisitokee tena.
Profesa Mdoe, akiagana na viongozi wa TANESCO baada ya ziara yake ya ghafla kwenye mitambo ya umeme wa Gesi, Kinyerezi jijini Dar es Salaam. (PICHA NA TANESCO)
Eneo la mitambo ya umeme wa Gesi Kinyerezi jijini Dar es Salaam
0 comments:
Post a Comment