Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya
Arusha, Lucia Mwiru akizungumza jijini A rusha katika Kata ya
Sekei. wakati alipokuwa akizungumza na wanachama, mabalozi
wa nyumba kumi, makatibu Kata,wazee maarufu
Na Mwandishi wetu Arusha
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha wametakiwa kuwaheshimu
mabalozi wa nyumba kumi wanaotokana na chama hicho ili kuleta maendeleo
ya kasi na yenye tija kwa wananchi hali ambayo itaongeza idadi ya
wanachama wapya
Pia wanachama hao wamesisitizwa kuacha majungu badala yake
kuhakikisha wanaimarisha chama kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali
sanjari na kufungua matawi na kugawa kadi mpya kwa wakati.
Hayo yalisemwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya
Arusha, Lucia Mwiru jijini A rusha katika Kata ya
Sekei. wakati alipokuwa akizungumza na wanachama, mabalozi
wa nyumba kumi, makatibu Kata,wazee maarufu
Alisema yeye ni
mgeni katika wilaya hiyo na ndio maana anapita kila Kata kwaajili ya
kuongea na wanachama wa CCM ikiwemo kuhakikisha kila jambo wanalolifanya
ni lazima mabalozi wa nyumba kumi waheshimiwe ikiwemo kushirikishwa
katika miradi mbalimbali ya chama.
Alikemea vikali tabia ya
baadhi ya wanachama kuwapuuza mabalozi na kuwaona wanamaana kwenye
chaguzi mbalimbali na mara ya chaguzi kuisha husaulika kabisa
.
Aidha
alisema kuwa mabalozi ni watu muhimu sana katika chama hivyo wanahaki
ya kuhusishwa katika miradi mbalimbali ya chama ili na wao wanufaike na
keki iliyopo badala ya watu wachache kukumbatia keki hiyo
Pia alisema
baadhi ya viongozi wa ccm wanafanya miradi ya chama kama shamba la bibi
huku wanachama pamoja na viongozi wengine hawajui nini kinaendelea na
hata wakihoji wanaambiwa kuwa ni wasaliti kwa kutengezewa maneno
yasiyofaa.
Naye Katibu wa
Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Mjini, Jasper Kishumbua alitoa rai
kwa wanachama wa chama hicho Mkoa wa Arusha na kata mbalimbali kuongeza
idadi ya wanachama pamoja na kufungua matawi ili kuongeza ari katika
chama
Kwa upande wa wanachama waliokuwepo katika mkutano huo , Nehemia Mollel na Mariam Hussein walitoa rai kwa
wanachama kujua wanachama wote wanaoishi kwenye kila Kata ili
panapotokea masuala ya uchaguzi iwe rahisi kuwajua kwani baadhi ya
wanachama wengine wanatoka Kata fulani kuja kupiga kura kwingine na
kupelekea chama kushindwa.
0 comments:
Post a Comment