MKUU wa
Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa
Na Rhoda
Ezekiel Kigoma,
MKUU wa
Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala ameahidi kuwachukulia hatua wasimamizi
wa miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa endapo watashindwa kukamilisha
miradi hiyo kwa wakati ilikuondoa upungufu wa vyumba vya
madarasa.
Maagizo
hayo aliyatoa jana wakati akikagua ujenzi wa madarasa manne na ofisi mbili
katika Shule ya Msingi Kakonko Wilayani humo ambapo alibaini kuwepo kwa tatizo
la ucheleweshwaji wa vifaa vya ujenzi kwa mafundi hali inayo pelekea kusua sua
kwa ujenzi huo.
Mkuu huyo
alisema mradi huo ulitakiwa kuwa umekabidhiwa lakini mpaka sasa mradi huo bado
haujakamilika kutokana na uzembe wa baadhi ya wasimamizi Wa mradi huo kushindwa
kuwasimamia mafundi ipasavyo waweze kukamilisha ujenzi huo, na ifikapo mwezi wa
tatu Mwishoni ujenzi huo uwe umekamilika
na wanafunzi wapate madarasa yao waendelee kuyatumia.
"
niwatake Wahandisi wa halmashauri kwa kushirikiana na Watendaji wa kijiji
kuwasimamia mafundi kwa karibu ilikuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati
endapo mtashindwa kusimamia ipasavyo tutawajibishana, Wananchi wamejitahidi
kuchangia na Serikali imetoa fedha kwa wakati ni lazima muhakikishe
mnakamilisha suala hili ilikuwatia moyo wananchi kuendelea kuchangia jitihada
za Serikali",alisema Kanali Ndagala.
Hata hivyo
Ndagala alisema katika Wilaya hiyo kunaupungufu wa madarasa ambapo mpaka sasa
juhudi za kumaliza changamoto hiyo inaendelea
kwa kuhakikisha Wananchi wanachangia kwa kushirikiana kujenga na
kufyatua tofari na serikali inasaidi a kiasi kidogo cha fedha pamoja na kuezeka
bati katika majengo hayo.
Kwa upande
wake Mkuu wa Shule ya Msingi Kakonko, Novatus
kalobagwa alisema Shule hiyo inazaidi ya Wanafunzi 1000 na ina madarasa
tisa ambapo matano yamekamilika na manne yanaendelea kujengwa , hali hiyo
inapelekea kila darasa kuwa na Wanafunzi 100-105 hali inayo pelekea mwalimu
kuwa na wakati mgumu katika ufundishaji.
Alisema
kutokana na Changamoto hiyo bado Wanafunzi katika shule hiyo wanaendelea
kufauru, ambapo mwaka jana Wanafunzi wote wa darasa la saba Walifauru kwa
asilimia miamoja na watano walipelekwa katika shule za vipaji maalumu kutokana
na ufauru wao kuwa mzuri.
Aidha
aliiomba serikali kihakikisha inamaliza kero hiyo kutokana na Maelekezo ya
elimu ni kwamba ilikuhakikisha Mwanafunzi anaelewa ni lazima darasa moja liwe
na Wanafunzi 45 kila chumba ambapo itamsaidia mwalimu kujua maendeleo ya
mwanafunzi mmoja mmoja na kuongeza ufauru kwa kiasi kikubwa.
0 comments:
Post a Comment