Waandishi wa habari wanawake kutoka mikoa mbalimbali nchini wakitembelea hifadhi ya Saadani.
Waandishi wa habari wanawake wakiwa katika hifadhi ya saadani iliyopo Mkoani Tanga na pwani yenye vivutio vya utalii wa kutembea kwa miguu,utalii wa boti,utalii wa fukwe za bahari ya Hindi na utalii wa kuwatembelea wanyama.
Akizungumza na waandishi waliopo kwenye ziara hiyo ya siku 10 mhifadhi utalii katika mbuga ya saadan ,Apaikunda mungule alisema kwa sasa watalii wanatakiwa kuja na Kadi ambazo hutolewa na benki za crdb ,Nmb pamoja na Exam bank.
Mungula alisema kuwa lengo la kutumia kadi hizo ni kukata kodi ya utalii pamoja na kuepusha usumbufu kwa watalii wanaofika katika hifadhi hiyo.
Hata hivyo mhifadhi huyo alisema kuwa hifadhi imetoa zaidi sh.mil.722 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya wananchi katika mikoa ya pwani na Tanga ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya,ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu,madawati 1500 ili kuweka mahusiano mazuri Kati ya wananchi na hifadhi .
Aidha mhifadhi huyo alisema kuwa hifadhi ambazo waaandishi wa habari wanawake wanaendelea kutembelea ni pamoja na ,Saadan,Udzungwa, Mikumi pamoja na Ruaha .
0 comments:
Post a Comment