Muanzilishi wa Taasisi ya Dorice Mollel, Dorice Mollel akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Novemba 16, 2016 juu ya matembezi ya hisani ya kuadhimisha Kilele cha Siku ya Mtoto Njiti Duniani, yanayotarajiwa kufanyika Novemba 19, 2016 Mjini Unguja Visiwani Zanzibar, ambapo Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mama Asha Balozi ndie anaetarajiwa kuyaongoza matezi hayo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu na kushoto ni Afisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano - UTT AMIS, Martha Mashiku.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Novemba 16, 2016, juu ya matembezi ya hiari yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya watoto njiti yanayotarajiwa kufanyika Mjini Unguja, Zanzibar mwishoni mwa wiki hii. Kulia ni Muanzilishi wa Taasisi ya Dorice Mollel, Dorice Mollel.
Afisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano - UTT AMIS, Martha Mashiku (kulia) akielezea namna walivyoshirikiana na Taasisi ya Dorice Mollel Foundation katika kufanikisha matembezi hayo.
*************
Na Bakari Madjeshi,Globu ya Jamii
Katika
kuhakikisha kuwa vifo vya Watoto Njiti vinapungua hapa nchini,Taasisi
ya Doris Mollel Foundation imeandaa Matembezi ya Hisani ili kukabiliana
na vifo vya watoto hao kupungua.
Matembezi
hayo yenye kauli mbiu ya "Okoa Maisha ya Mtoto Njiti" yatafanyika
Visiwani Zanzibar kutokana na Wanawake wengi visiwani humo kukabiliwa
kwa asilimia kubwa na suala hilo la Watoto kuzaliwa Njiti.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mwanzilishi wa Taasisi
hiyo, Doris Mollel amesema kuwa Watoto wengi wanakufa kutokana na
kushindwa kupumua wenyewe, hivyo wao kama Taasisi imewasukuma kusaidia
suala hilo.
Dorice
ametoa shukrani kwa Wadhamini waliojitolea kuasaidia kukabiliana na
suala hilo ikiwa ikiwa ni Vodacom Foundation Tanzania, GSM Foundation,
Clouds Media Group na UTT AIMS, Michuzi Media Group na wengine wengi.
Pia
ametoa shukrani kwa Viongozi wa Serikali kama Mhe. Angela Kairuki, Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, Wizara za Afya Tanzania Bara na Visiwani.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Vodacom Tanzania, kupitia kwa Mkuu wa Kitengo
cha Mahusiano na Mwasiliano, Jacquiline Materu amesema wameamua
kudhamini Kampeni hiyo ikiwa ni fursa nzuri kuondoa vifo vya Mama na
Mtoto.
Naye
Afisa Mwandamizi Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS amesema wanashirikiana
Doris Mollel Foundation toka mwaka Jana amesema watasaidia Kampeni hiyo
ya Okoa Mtoto Njiti kuhakikisha wanapunguza vifo vya akina mama na
Mtoto.
0 comments:
Post a Comment