Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip Mpango (kushoto) pamoja na mkuu wa chuo hicho Prof. Innocent Ngalinda (kulia) kuingia ukumbini pamoja na wahitimu tayari kwa mahafali.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua mahafali ya pili yaliofanyika chuoni hapo.
Sehemu ya Wahitimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika.
Mgeni
Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha
Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtunuku mmoja wa wahitimu kati ya wahitimu 133 waliohitimu leo na kutunukiwa Shahada na Stashahada.Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Sudan Mhe.Mahgoub Ahmed Sharfi , ambapo mabalozi mbali mbali walihudhuria. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja Mabalozi wa nchi mbali mbali waliohudhuria mahafali hayo.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekiri kuwa Wizara,
Idara na taasisi za Serikali zina matumizi madogo ya takwimu sahihi
zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini hali ambayo inachangia kurudisha nyuma shughuli
za upangaji wa maendeleo za wananchi.
Makamu wa
Rais wa Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo trh 19-Nov-2016 katika hotuba yake kwenye mahafali ya Pili ya Chuo cha
Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC)
Jijini Dar es Salaam.
Kutokana na
hali hiyo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu
Hassan ameziagiza wizara, Idara na taasisi za Serikali kuimarisha matumizi ya
takwimu sahihi kwa ajili ya kupanga na kuweka mikakati ya kuwaletea wananchi
maendeleo endelevu.
Makamu wa
Rais ameutaka uongozi wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika uimarishe
ushirikiano na Wakuu wa Takwimu wa Afrika kwa kuhakikisha watakwimu wanaoingia
katika soko la ajira wanafanya kazi zao kwa kufuata misingi ya kisheria na
kanuni zake katika ukokotoaji wa takwimu zinazokubalika kitaifa na kimataifa
ambazo zitawezesha Afrika kupanga maendeleo ya wananchi kwa ufanisi mkubwa.
Amewahimiza
wahitimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika pindi watakapoanza kufanya
kazi zao wafanye kazi kwa ufanisi na kwa umakini wa hali ya juu ili kutimiza
azma ya kutokomeza kabisa umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2030 katika bara
la Afrika.
“Wito wangu kwa Wizara, Idara na
Taasisi za Serikali kuhakikisha zinaimarisha vitengo vya takwimu kwa kuwaruhusu
maofisa waliopo katika vitengo vyao vya sera na mipango wapate fursa ya
kupatiwa mafunzo elekezi na ya muda mfupi kwa ajili ya kuongeza ujuzi wao wa
kuchambua na kukokotoa takwimu rasmi”
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa hategemei kuona wahitimu walio maliza
masomo yao katika ngazi mbalimbali katika Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika
wamalize soli za viatu kusaka ajira na kwamba Serikali itawawekea mazingira bora
ya kupata ajira haraka.
Kwa upande
wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango amesema Serikali itaendelea
kushirikiana kikamilifu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kutumia takwimu
sahihi ambazo zimetolewa na ofisi hiyo katika kupanga shughuli za maendeleo za
taifa.
Katika
mahafali hiyo ya Pili ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika, Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewatunuku vyeti
wahitimu 133 katika ngazi za Shahada ya Uzamili ya Takwimu, Shahada ya awali ya
takiwmu na Stashahada ya takwimu kwa wahitimu kutoka nchi Kumi za Afrika ambazo
ni Nigeria,Ghana,Sierra Leon, Ethiopia,Somalia, Uganda, Swaziland, Liberia,
Rwanda na mwenyeji Tanzania.
0 comments:
Post a Comment