MGOMBEA Ubenge Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amewashinda wagombea wenzake saba kutoka vyama vya CCM, AFP, DP, NRA, SAU, UPDP na TLP katika uchaguzi mdogo wa Ubunge uliofanyika Aprili 1, 2012.
Kwa Mujibu wa Matokeo ya liyotangazwa asubuhi hii yanaonesha kuwa Mgombea Ubunge wa 32,972 26,757.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Arumeru Bw Gracias Kagenzi amemtangaza mgombea wa CHADEMA Bw Joshua Nassari kuwa mshindi.
Gagenzi pia ametangaza matokeo ya wagombea wengine ambao walitoka vyama vya Siasa nchini kuwa kama yafuatavyo:-
AFP – 139, DP -77, NRA – 35, SAU – 22, UPDB – 18 na TLP – 18.
Kwa mujibu wa Bw Kagenzi zaidi ya watu 120,000 walijiandikisha na aliojitokeza na kupiga kura walikuwa 60,696 ambapo kura halali zilikuwa 60,038 na zilizoharibika ni kura 661.
Aidha CHADEMA pia jana katika Uchaguzi wa Udiwani imepata Ushindi katika Kata za Kirumba mkoani Mwanza na Kiwira mkoani Mbeya.
safi sana wanameru kuonyesha ushirikiano kwa chama cha maendeleo,chadema oyeeeeeeeeeeeeeeee
ReplyDeleteHICHO NDICHO WALICHO PANDA CCM WANAKIVUNA SASA
ReplyDeleteGod bless Tanzania God bless Chadema with his new MP.Joshua Nasari!
ReplyDeleteWana Arumeru tunafuraha isyo kifani kwa ushindi tulioupata ...Tunakutakia kila la heri mbunge wetu JOSUA NASSARI... Chadema hoyeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!
ReplyDeletethese are changes that are needed in this country...
ReplyDeleteSisi tunamwomba Mungu wetu wa Mbinguni,wao wanatumia vyeo na pesa zao Za kifisadi,yako wapi si niliwambia???N bado mwaka 2015 itakuwa balaa kwa ccm.
ReplyDeleteMungu ibariki Tanzania,bariki Chadema.
Hii ni red alert kwa CCM, ili ushinde sasa ukiwa mgombea wa CCM unahitaji juhudi zako binafsi na si za chama kama ilivyokuwa zamani, zamani ukiteuliwa tu kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM basi unahesabu ushindi asilimia 100. Kwa sasa sivyo kwani CCM imegawanyika kila mmoja ana msimamo wake eti uhuru wa kutoa mawazo haukuwepo huo wakati wa Baba wa Taifa, CCM ilikuwa moja, mawazo, kauli, maamuuzi, msimamo na kila kitu kwasasa mambo ni vululu vululu.
ReplyDeleteWatafute mahali pa kukimbilia,haswa wahamie kwenye nymba zao ulaya maana wembe wa Arumeru utakuwa mkali zaidi mwaka 2015.PEOPLES POWER.
ReplyDeletehakuna marefu yasiyokuwa na ncha, CCM mrudieni Mungu!
ReplyDeleteHata hivyo CCM mmejitahidi keep it up ila mjitahidi acheni uchakachuaji miaka 50 bado tu. embu tuwape hawa vijana nao tuwaone wakichemsha si uchaguzi unaofata tutawatosa !!!
ReplyDeletea great day for Arumeru and democracy for tanzania.A time has come where money,bigwigs,power etal is no match to peoples'power.
ReplyDeleteLong live democracy.
CHADEMA JUU TUMECHOKA KUONEWA NA MAFISADI WA ...........
ReplyDeleteMimi nilishangaa pale UHURU FM walipokataa waligoma kusoma habari za ushindi wa Nassari. Katika mapitio ya magazeti walijidai eti "uchaguzi umekwisha sasa haya yote ya nini". Siku ya pili waliharakisha kusoma habari za Nape kukubali kushindwa. Huo ndio weledi wao
ReplyDeletemimi nimefurai sana kuona chadema wamechukua kiti hiki cha arumeru,mashariki,ila watanzania tuna hali ngumu sana kwa sasa, namaanisha hatuna uhuru uliokamilika, tunatawaliwa na watu kutoka nchi za uchina na india kirahisi sana. watanzaia wengi twapaswa kuamka kupitia chama hiki kukataa hili. kufanya kazi kwetu ndo ukuaji wa uchumi wetu itakuaje hawa wakoloni ndo tuwakaribishe katika ukuaji wa uchumi wetu, matokeo yake wanachangia kidogo sana, na kulipa wafanyakazi mishahara kidogo, na hao wafanyakazi ni vijana sasa tanzania itafika lini?
ReplyDeleteCHADEMA CHAMA MAKINI, wakati ujao ni zamu ya Tabora kwa maana ei mbunge wetu anaishi dar na juzi kaenda setif naye tumemchoka hana lolote bora andelee kuanya kazi simba kwa maana inampendeza sana na ninamkubali awapo simba mmi kama shabiki wa simba ila ubunge ameproof failure.
ReplyDeleteTabora hamna hata barabara ya lami hata tu hapa manispaa!duh..ccm chini
Chadema safi sana ndugu
ReplyDeleteJoshua samweli nassar kwa kuchaguliwa kuwa mbunge wa meru mashariki mungu akubariki na akupe hekima na maarifa katika kuhudumia wananchi wako