Wahitimu wakiimba shairi kwa
mgeni rasmi (hayupo pichani) katika Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe
leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha VETA,
Chang’ombe, Douglas Kipokola akitoa maelezo katika mahafali ya 46 ya chuo
hicho leo jijni Dar es Salaam.
sehemu
ya wahitimu wakati wa Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe leo jijini
Dar es Salaam.
Sehemu ya wazazi katika
Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu VETA ,
Geoffrey Sabuni akitoa cheti kwa mmoja wa wahitimu katika Mahafali ya 46 ya
Chuo cha VETA, Chang’ombe leo jijini Dar es Salaam.
***********
NCHI inakwenda katika uchumi
wa viwanda ambavyo vinahitaji wataalam mbalimbali katika kuweza
kufikia uchumi huo kwa kuhitaji wataalam wanaozalishwa nchini wakiwemo
wahitimu wa mafunzo stadi yanayotolewa na vyuo vya VETA.
Hayo ameyasema leo na Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi Stadi
(VETA), Geoffrey Sabuni wakati wa mahafali ya 46 katika Chuo cha
VETA, Changombe Dar es Salaam, amesema VETA inazalisha wataalam
ambao wamebobea kwa ujuzi.
Amesema wahitimu wa VETA
hawatafuti ajira kutokana na kuwa ujuzi wanaoupata unawawezesha
kujiajiri au kuajiriwa kwa kutafutwa na wamekuwa wakifanya vizuri katika maeneo
walioajiriwa na kujiajiri.
Sabuni amesema wanaosoma
VETA wapo waliohitimu kidato nne hadi waliopata shahada ya kwanza
hivyo jamii iondoe dhana ya kwamba wanaosoma VETA ni wale walioshindwa
kufanya vizuri katika shule za sekondari na msingi.
Aidha amewataka wahitimu
wanaozalishwa na vyuo hivyo kuwa na weledi katika kufanya kazi na
kuondokana kuwaibia waajiri hali ambayo itafanya baadhi yao kupoteza sifa ya
kujiajiri au kuajiliwa.
Nae Mkuu wa Chuo cha
VETA Changombe, Douglas Kipokola amesema kuwa wahitimu mwaka huu
wako 423 katika fani mbalimbali na kwamba wapo tayari katika soko la
ajira kutokana na mafunzo walioyapata.
Amesema kuna changamoto
za walimu ambapo wameshaanza kulifanyia kazi kutokana na mitaala
inahitaji mafunzo yenye tija kwa uwiano wa mwalimu mmoja kwa
wanafunzi wasiozidi 20.
0 comments:
Post a Comment