Nafasi Ya Matangazo

October 07, 2016

Wakuu wa Wilaya wakiwasili kwenye Mtambo wa Maji wa Ruvu juu Mlandizi, Mkoani Pwani. 
 
KATIKA ziara iliyoandaliwa na Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO) kwenye mitambo ya uzalishaji Maji ya Ruvu juu na Ruvu chini pamoja na katika miradi inayoendelea kwa wakuu wa wilaya zote za jijini la Dar es salaam pamoja na Pwani yenye lengo lakuonyesha hatua zinazofanywa kuboresha huduma ya Majisafi.

Akizungumza kwenye ziara hiyo Afisa mtendaji mkuu wa DAWASCO mhandisi Cyprian Luhemeja ameeleza lengo la kuwaleta wakuu hao wa wilaya kwenye miradi inayoendelea kuwa ni kuonyesha hatua ambazo shirika linafanya la kuongeza upatikanaji wa majisafi jijini Dar es Salaam.
 
‘’lengo la ziara hii ya leo nikutembelea miundombiu ya dawasco ili kuweza kuboresha huduma ya maji safi katika jiji la Dar es salaam na kuwaondolea kero wananchi juu ya uhaba wa huduma hii ya maji ili kuweza kuboresha hali zao, sisi kama dawasco tuna kauli mbiu ya mama tua ndoo kichwani ambapo kauli mbiu hii inalenga kumtua ndoo mama kichwani’’alisema Afisa Mtendaji wa Dawaasco Cyprian Luhemeja.
 
Luhemeja aliwataka wananchi kutunza miundombinu ya shirika hilo ili kuwawezesha wakinamama ambao wanamchango kubwa katika kuihuhudumia jamii kuweza kuwatua ndoo kichwani kuendelea na shughuli nyinginezo za kuihudumia jamii.
Meneja wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa akitoa maelezo mafupi kwa wakuu wa Wilaya za Dar es salaam na Pwani leo katika ziara iliyoandaliwa na Shirika la Majisafi na Majitaka (Dawasco).
Afisa mtendaji mkuu wa DAWASCO mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya za Dar es salaam na Pwani, wakati wa ziara iliyoandaliwa na Shirika la Dawasco.
Posted by MROKI On Friday, October 07, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo