Kamanda
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga akipokea moja ya stika
zilitolewa na TPB kutoka kwa Meneja Masoko na Uendeshaji wa TPB, Deo Kwiyukwa
Kamanda
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga, Meneja Masoko na
Uendeshaji wa TPB, Deo Kwiyukwa pamoja na Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya TPB,
Timotheo Mwakifulefule wakionyesha stika hizo kwa vyombo vya habari.
Kamanda
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga akibandika stika hizo
katika moja ya gari la abiria katika stendi ya mabasi yaendayo mikoani, Ubungo.
Kulia niMeneja Masoko na Uendeshaji wa TPB, Deo Kwiyukwa
Meneja
Masokona Uendeshaji wa TPB, Deo Kwiyukwa akiongea na vyombo vya habari, baada
ya kutoa stika za kwenda kwa usalama barabarani
Kamanda
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga akiishukuru TPB wakati
akiongea na vyombo vya habari.
Kamanda
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga akitoa maelekezo juu ya
matumizi sahihi ya stika hizo kwa viongozi wa Kikosi cha usalama barabarani
pamoja na wakuu wa Chama cha Kutetea Abiria (CHAKUA) BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Kamanda
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga akipokea
zawadi ya TPB kutoka kwa Meneja Masoko na Uendeshaji wa TPB, Deo Kwiyukwa.
*****************
BENKI
ya Posta Nchini (TPB) imetoa msaada wa stika zaidi ya 2,000 zenye namba za
Wakuu wa Usalama Barabarani wa Mikoa yote nchini zitakazobandikwa kwenye mabasi
yaendayo mikoani.Huu ni mwaka wa nne mfululizo benki hiyo anatoa stika hizo kwa
lengo la kupunguza ajali katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa mwaka.
Akizungumza
wakati wa kubandika stika walizozipokea katika mabasi hayo, Kamanda Mkuu wa
Usalama Barabarani Mohammed Mpinga, aliwataka madereva kuendelea
kuzingatia Sheria na kanuni za usalama barabarani ili kutokomeza ajali
zinazoendelea kupoteza maisha ya watu wengi.Alisema ofisi yake ilikuwa inapokea
maombi mengi kutoka kwa wananchi ili kupata namba zitakazowawesha kutoa taarifa
za madereva wanaofanya makosa wakiwa safarini.
Alisema
kuwa stika hizo zitabandikwa katika mabasi yote yaendayo mikoani pamoja na yae
madogo maarufu kama Coastal.
"Tunaishukuru benki ya Posta kwa msaada huu kwani wametupa muda muafaka wa
kuelekea mwishoni mwa mwaka ambapo kumekuwa na ajali nyingi sana zinazopoteza
maisha ya watu wengi na kuwaacha wengine na ulemavu wa kudumu", alisema
Kamanda Mpinga.
Aliongeza
kuwa Kitengo chake kitaendelea kushirikiana na TPB na wadau wengine kuhakikisha
wanaendesha kampeni hii na kutokomeza kabisa ajali za barabarani.
Akikabidhi
msaada huo Meneja Masoko na Uendeshaji wa TPB, Deo Kwiyukwa alisema kuwa lengo
la kutoa stika hizo ni kupunguza ajali na kupoteza nguvu kazi ya Taifa katika
kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa mwaka.
Alisema
kwa kipindi cha miaka minne iliyopita toka waanze kampeni hiyo ajali nimeweza
kupungua kwa kiasi kikubwa kutokana na madereva kuhofia kuripototiwa na abiria
katika vyombo vya Usalama ambapo itapelekea kusimamishwa, faini kali au kifungo.
Deo aliwataka abiria kutumia vema
namba hizo za simu kwa lengo lakudhibiti mwendo mkali na kutokomeza kabisa
ajali hizo."TPB napenda kuwaasa watumiaji wa mabasi ambao wengi ni wateja
wetu kutoa taarifa katika vyombo vya Usalama pale madereva wanaofanya makosa
hasa.
Naye
Afisa elimu kutoka Chama cha Kutetea Abiria (CHAKUA), Gervas Rutagunziga
alisema kuwa viashiria vya ajari ni vingi sana lakini wananchi hawapo katika
sehemu sahihi ya kulisemea jambo hilo, hivyo basi TPB inawapa nafasi kwa abiria
kuokoa maisha yao kwa kupiga simu pale ambapo wanakuwa hawaridhishwi na mwendo
kasi wa dereva au hali ya dereva kama amelewa au hajalewa.
"Mara
nyingi abiria wamekuwa na uwezo wa kuzuia ajali lakini wanashindwa kufanya
hivyo kutokana na kutojua watafikisha vipi taarifa katika vyombo husika, hivyo
tunaamini kupitia stika hizi zenye namba za simu abiria sasa watakuwa na uwezo
mkubwa zaidi wa kulinda maisha yao" alisema Rutagunziga.
0 comments:
Post a Comment