Nafasi Ya Matangazo

October 06, 2016

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) inaendelea na kongamano lake la kimataifa la Wanasayansi watafiti la 30 jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa mambo mengi ambayo yajnajadiliwa ni pamoja na namna ya kuweza kuhamasisha na kusaidia watoto wa kike nchini kuweza kusoma masomo ya sayansi na kuwapa hamasa za kuweza kutimiza ndoto zao kufikia malengo hayo.

Wanawake wanasayansi watafiti walikutana na kujadili namna yakuweza kusaidia kuleta hamasa kwa watafiti chipukizi na wale walioko shulebni kuweza kuvutiwa na masomo ya sayansi na kusoma kwa bidii.

Pichani juu ni Mwanasanasi Mtafiti Mwandamizi na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Amani Tanga, Dk Theresia Nkya akielezea chagangamoto mbalimbali alizokumbana nazo na namna alivyoweza kuzikabili hadi kutimiza malengo yake.

Mwisho wa mdahao huo watafiti hao kila mmoja aliweka ahadi yake kimaandishi jinsi ambavyo atasaidia kwa nafasi yake wale ambao wanachipukia na kutaka kuchukua masomo ya sayansi waje kuwa watafiti. 

Aidha watafiti hao wanasayansi wanawake wametaka kuwepo na mikakati endelevu ya kuweza kuwasaidia wanasayansi chipukizi ili uhamasishaji unaofanyika mashu;leni kuwataka watoto wakike kusoma masomo ya sayansi uwe na mafanikio na kuleta tija. 


Msikilize hapa Dk Theresia Nkya
Mwanasayansi Mtafiti kutoka NIMR Makao Makuu, Basiliana Emidi nae akitoa ushuhuda wake kwa yale aliyopitia na anayopitia na ushauri wake kwa wanasayansi wanawake chipukizi.
Mwanasayansi Mtafiti Mstaafu, Dk Edith Lyimo nae alipata wasaa wa kuzungumza na kuelezea yale aliyokumbana nayo wakati akifanya tafiti mbalimbali na jisni alivyofanya kazi zake na wanaume miaka ya 1980. 

Dk Nkya aliwataka wanasayansi watafiti chipukizi kuto kata tamaa na badala yake kuhakikisha wanafikia malengo yao kikamilifu.
Tunu Mwinyimbegu (katikati) ni mmoja kati ya wasichana ambao wanandoto za kuwa wanasayansi watafiti licha ya kuwa alikuwa na vitu vingine alivyokuwa akifikiria kuvifanya katika maisha yake kama vile kuwa msanifu kurasa akieleza ndoto zake na watu wanaompa hamasa. Kulia ni Lucy Mrema na kustoto ni Mary-Angel Jimmy wote kutoka Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mahakama ya Makosa ya Jinai (MICT).
Mary-Angel Jimmy wote kutoka Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mahakama ya Makosa ya Jinai (MICT) akielezea ndoto zake za kuwa mwanasayansi na watu wanaomsukuma kutimiza ndoto hizo. 
 Watafiti mbalimbali wakifuatia mada katika mdahalo huo.
Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt Mwele Malecela akifuatilia kwa makini mjadala huo ambapo watafiti wa ngazi mbalimbali walikuwa wakielezea namna ambavyo wanakabiliana na chanagamoto katika kazi zao na jinsi walivyo weza kuvuka vikwazo na kufikia malengo yao.
 Wanafunzi Rozina Robert wa kidato cha sita mchepuo wa Sayansi (PCB) Shule ya Sekondari Tambaza (kulia) na Janeth Vegula wa kidato cha kwanza Sekondari ya Canossa wakifuatilia hamasa waliyokuwa wakipewa. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

 Watafiti wakifuatilia
 Wanafunzi Rozina Robert wa kidato cha sita mchepuo wa Sayansi (PCB) Shule ya Sekondari Tambaza akielezea jinsi ambavyo anapenda masomo ya sayansi na anavyotaraji kuwa hapo badae.
 Janeth Vegula wa kidato cha kwanza Sekondari ya Canossa yeye anasema kuwa matarajio yake ni kuwa mfanyabiashara hivyo anataka kusoma biashara ila kwa hamasa aliyoipata hapo anaweza hamia huko maana anasema amefundishwa kucheza mziki kulingana na midundo yake.
 Caroline Senga yeye ni mwanafunsi wa masuala ya Saikolojia na yupo NIMR kwa mafunzo.
 Historia ya Mwanasanasi Mtafiti Mwandamizi na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Amani Tanga, Dk Theresia Nkya iliwavutia wengi na kutaka kujua zaidi.
Watafiti wakimsikiliza Dk Theresia Nkya.
Mwisho kila mtafiti aliyeshiriki kwa nafasi yake aliahidi nini acha kufanya katika kusaidia wasichana wanaotaka kusoma sayansi na kuwa watafiti.
Posted by MROKI On Thursday, October 06, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo