Rais Dk John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya Wafanyakazi
katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani
zulizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na viongozi wa
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi TUCTA wakati wakiimba wimbo wa Mshikamano
Daima katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani
zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma .
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwenye banda la
Wakala wa Afya na Usalama mahala pa kazi OSHA mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa TUCTA Gratian Mukoba wakati alipowasili
katika katika viwanja vya Jamhuri Mkoani Dodoma. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuagana na mamia ya
wafanyakazi katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kuwa serikali yake itapunguza kodi
katika mishahara ya wafanyakazi kutoka asilimia 11 hadi kufikia asilimia 9
kuanzia mwaka ujao wa fedha wa 2016/2017 ili kupunguza mzigo kwa wafanyakazi.
Rais Magufuli ametangaza
uamuzi huo leo tarehe 01 Mei, 2016 wakati akihutubia katika sherehe za
maadhimisho ya siku ya siku ya wafanyakazi duniani, zilizofanyika kitaifa
katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
"Napenda kuwataarifa kuwa
serikali yangu kama nilivyoahidi wakati wa kampeni zangu, nimeamua kupunguza
kodi ya mapato ya mishahara kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 9, kuanzia
mwaka wa fedha wa 2016/2017, nikiwa nina mategemeo makubwa waheshimiwa wabunge
watapitisha bajeti ya serikali niliyoiwasilisha" Amesema Dkt. Magufuli
huku akishangiliwa na maelfu ya wafanyakazi waliojitokeza uwanjani hapo.
Pamoja na uamuzi huo, Rais
Magufuli pia amewaahidi wafanyakazi kuwa baada ya kupunguza kodi katika
mishahara ya wafanyakazi, serikali yake itafanyia kazi mapendekezo ya kuongeza
mishahara.
Katika maadhimisho hayo ambayo
pia yamehudhuriwa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu
Mheshimiwa Kassim Majaliwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Akson, Rais Magufuli
amewataka wafanyakazi kote nchini kushiriki kufanikisha Dira ya Maendeleo ya
Taifa ya 2025 kwa kufanya kazi kwa bidii, kujituma, weledi na uadilifu.
Amesema Mpango wa Maendeleo ya
Taifa utagharimu takribani shilingi Trilioni 107 zikiwemo shilingi Trilioni 59
kutoka serikalini, hivyo amewataka wafanyakazi wote kutambua kuwa wanategemewa
kuwaongoza watanzania kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo kwa kuchapa kazi.
Aidha, Rais Magufuli amewataka
wafanyakazi kuunga mkono juhudi za kuwafichua wanaozalisha wafanyakazi hewa,
huku akibainisha kuwa mpaka kufikia jana tarehe 30 Aprili, 2016 jumla ya
wafanyakazi hewa waliobainika walikuwa 10,293 ambao kwa mwezi mmoja tu wamelipwa
shilingi bilioni 11.6.
"Kwa hiyo kwa mwaka wafanyakazi
hewa hawa wamekuwa wakilipwa shilingi 139,239,285,592.92, ukizidisha kwa miaka
mitano kama tungekuwa na wafanyakazi hewa, miaka mitano tu, tusiseme miaka kumi
au ishirini au kumi na ngapi, miaka mitano tu, manaake wangelipwa shilingi
696,196,427,964.6.
"Hizi bilioni 696
zinatosha kujenga madaraja kama la Nyerere lililopo Kigamboni, madaraja matatu,
hizi bilioni 696 zinatosha kujenga flyover zinazojengwa Dar es salaam kwa
msaada na mkopo kutoka Japan, zingekuwa saba, hizi bilioni 696 mjiulize kama
zingetumika kulipa mishahara ya wafanyakazi waliopo ndani ya serikali,
tungewaongezea mshahara kiasi gani" amesisitiza Rais Magufuli.
Hata hivyo Rais Magufuli
amewahakikishia wafanyakazi wote ambao wanatekeleza majukumu yao kihalali kuwa
serikali yake itawalinda na kuwatetea huku akitaka wawapuuze wanaodai serikali
ya awamu ya tano haiwapendi wafanyakazi.
"Tukumbuke ya kuwa kazi
ni utu, kazi sio fursa ya kupata mshahara kwa manufaa ya familia zetu bali ni
fursa nzuri ya kutoa mchango kwa taifa lako kwa manufaa ya kizazi cha sasa na
kijacho" amesema Dkt. Magufuli.
0 comments:
Post a Comment