Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (Kushoto), akikabidhi vifaa vya usafi kwa mmoja wa wakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (kulia), ikiwa ni sehemu ya msaada wa vifaa vya kufanyia usafi katika jiji la Dodoma, walivyowakabidhiwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, hapo jana. Wanaoshuhudia (kutoka kulia) ni Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao akifuatiwa na meneja masoko wa Airtel Dodoma Hendrick Bruno na wanakikundi wa Pambana wapatao vijana 30 na walezi wa kikundi hicho.
Mwakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (kulia), akiwa mwenye furaha baada ya kukabidhiwa na Airtel Tanzania, msaada wa pikipiki 2 za magurudumu matatu aina ya Toyo, malighafi na vifaa mbali mbali vya shughuli za usafi, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika katika eneo lao la biashara Majengo jijini Dodoma hapo jana.Akishuhudiwa na Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki (kushoto),akifuatiwa na meneja masoko wa Airtel Dodoma Hendrick Bruno na Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao.
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kati), akikabidhi vifaa vya usafi kwa mmoja wa wakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (wanne kulia), ikiwa ni sehemu ya msaada wa vifaa vya kufanyia usafi katika jiji la Dodoma, walivyowakabidhiwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, waliopo Majengo jijini Dodoma hapo jana. Wanaoshuhudia (wane kulia) ni Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao na wanakikundi wa Pambana wapatao vijana 30 na walezi wa kikundi hicho. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Diwani wa kata ya Majengo Dodoma, Msinta Mayaoyao (pili kushoto) akitoa maneno machache katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa vya usafi ambapo kikundi cha Pambana kilikabidhiwa msaada wa pikipiki 2 za magurudumu matatu aina ya Toyo, malighafi na vifaa mbali mbali vya shughuli za usafi, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, hapo jana. Akisikilizwa na afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kati), Meneja masoko wa Airtel Dodoma Hendrick Bruno (kulia) na wanakikundi wa Pambana wapatao vijana 30 na walezi wa kikundi hicho.
Mwakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (pili kulia) kilichopo Majengo Dodoma akiwa mwenye furaha baada ya kukabidhiwa funguo ya pikipiki aina ya Toyo na afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki, (tatu kushoto), kwa ajili ya shughuli zao za usafi, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika katika eneo lao la biashara Majengo jijini Dodoma hapo jana.
******************
PAMBANA ni kikundi cha vijana
30 wajasiriamali kinachojishughulisha na shughuli mbalimbali katika jamii
kama kukusanya taka, kuzalisha na kusambaza sabuni na kuchomelea vyuma mjini
Dodoma, ambao leo wamepokea vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 17 kutoka
Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel FURSA. Kundi hili limepokea vifaa
mbalimbali vikiwemo pikipiki mbili aina ya Guta, sare za kufanyia kazi,
mabuti, reki ya chuma, ufagio mgumu na vifaa vingine vya usalama vya
kufanyia kazi zao.
Afisa uhusiano wa Airtel,
Dangio Kaniki aliwapongeza kikundi cha Pambana kwa juhudi zao na kufanya kazi
kwa bidii. Akizungumza katika hafla ya makabidhiano alisema, " Tumeamua
kutoa vitendea kazi vya usafi ili kuweza kuungana na kikundi hiki katika kufikia
lengo kuu la kuhakikisha maeneo yanayozunguka jamii yanakuwa katika hali ya
usafi na hivyo kuchangia katika mikakati ya kutunza mazingira kwa ujumla.
Sambaba na hili Airtel imeona
nia na juhudi zao kikundi hiki na ndio maana leo imewakabidhi vifaa vitakavyowawezesha
kufanya kazi kwa haraka na kukuza biashara yao".
"Kikundi cha Pambana
kimeshapata mafunzo ya biashara ya ujasiriamali kupitia Airtel FURSA na
wataendelea kupata ushauri na uongozi kutoka kwa washauri wa Airtel FURSA ili
kuwawezesha kuimarisha biashara yao " aliongeza Kaniki
"Kama kampuni ya simu
inayojali jamii yake, tumeahidi kuwawezesha vijana hapa nchini kwa
kuwawezesha kwa njia mbalimbali ili waweze kufikia ndoto zao." alisema
Kaniki.
Kwa upande mwingine kundi la
Pambana waliahidi kuweka ujuzi wao wote na kutumia kwa umakini vifaa
vilivyotolewa kwao na Airtel kwa matumizi bora na yaliyo sahihi.
Kiongozi wa kikundi hicho,
Amasha Zuberi, aliishukuru Airtel kwa msaada na kutoa wito kwa mashirika
mengine hapa nchini kuuunga mkono mpango wa Airtel katika kusaidia vijana
zaidi katika Jamii.
"Hatukuamini siku moja
tutakuwa na uwezo wa kufikia malengo yetu katika biashara hii, tunaahidi kuweka
juhudi zaidi na kutumia vifaa hivi na mafunzo tuliyopata kwa umakini zaidi
kuhakikisha tunainua zaidi biashara yetu," alisema Amasha.
Kwa upande wake, wakati wa
hafla ya makabidhiano, Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao alitoa wito
kwa vijana kutumia program hiyo ya Airtel Fursa kujiendeleza. Huku akiwaomba
watanzania kuwapendekeza vijana wote wanaoona wanafaa kufaidika kwa mradi huo
kwa manufaa ya jamii zao kwani Airtel FURSA ipo kwa ajili ya kubadilisha maisha
ya vijana hapa nchini.
Airtel FURSA, inazunguka nchi
nzima kukutana na vijana kwa lengo la kuwapa elimu ya ujasiriamali na kisha
kutoa uwezeshaji kwa vijana ili kuhakikisha kuwa wanafikia ndoto zao.
Ili kijana kushiriki au
kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15626 na
kuweka maelezo yafuatayo:- Jina, Umri, aina ya biashara na eneo.
Pia wanaweza kutuma maombi yao
kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com.
ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, aina ya biashara na sababu ya
kuomba msaada kutoka Airtel.
0 comments:
Post a Comment