Nafasi Ya Matangazo

August 10, 2026

Timu ya mpira wa miguu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya imeibuka bingwa wa mashindano ya mpira wa miguu kanda ya nyanda za juu kusini baada ya kuwafunga goli moja kwa bila Polisi Mkoa wa Songwe.


Akizungumza mara baada ya fainali hiyo iliyochezwa Agosti 10, 2026 Mkoani Rukwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga amesema kuwa ushindi huo umetokana na maandalizi mazuri ya timu, umoja na mshikamano.

Aidha, Kamanda Kuzaga amewapongeza wachezaji, benchi la ufundi na vikundi vya hamasa kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake hadi kupata matokeo mazuri na kusisitiza nidhamu kuelekea maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 20 ya Polisi Jamii ambapo timu hiyo itashindana na timu kutoka kanda nyingine.

Mashindano hayo ya kikanda yalifunguliwa rasmi Agosti 09, 2026 yalishirikisha timu za mpira wa miguu, mpira wa pete, riadha, kuvuta kamba na michezo mingine ya jadi ikijumuisha mikoa ya Rukwa (Mwenyeji), Mbeya, Songwe na Katavi ikiwa ni maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 20 ya Polisi Jamii yatakayofanyika Agosti 25, 2026 Mkoani Mbeya yakibeba kauli mbiu inayosema, Miaka 20 ya Polisi Jamii: Tushirikiane kuimarisha Amani, Usalama na Umoja wa Kitaifa.






 

Posted by MROKI On Monday, August 10, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo