Na Neema Chalila Mbuja, DodomaRAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 8, 2026 amefunga rasmi Maonesho ya NANE NANE yaliyokuwa yakifanyika kwenye Viwanja vya Dkt John Malecela Nzuguni Dodoma na kuwapongeza Wizara ya Kilimo , Mifugo na Uvuvi kwa kazi nzuri liliyofanya kuwaunganisha wadau wa kilimo kwenye maonesho hayo.
Katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii maelfu ya wananchi wamefurika kwenye bustani ya wanyamapori hai ili kujionea wanyama mbalimbali.
Sambamba na hilo viongozi mbalimbali wa Wizara ya Maliasili na Utalii wametembelea banda la Wizara hiyo kwenye Viwanja vya NANE NANE kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika na taasisi na wadau wa Malikale, Misitu na Nyuki, Utalii na Wanyamapori.
Wakiwa kwenye Maonesho hayo walipata fursa ya kuzungumza na wananchi na wadau na kueleza mustakabali wa sekta ya utalii sambamba na mikakati iliyojiwekea kwa ajili ya kutangaza sekta ya utalii hususani katika kipindi hiki cha kuelekea Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.
















0 comments:
Post a Comment