Nafasi Ya Matangazo

May 01, 2016

Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (Kushoto), akikabidhi vifaa vya usafi kwa mmoja wa wakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (kulia), ikiwa ni sehemu ya msaada wa vifaa vya kufanyia usafi katika jiji la Dodoma, walivyowakabidhiwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, hapo jana. Wanaoshuhudia (kutoka kulia) ni Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao akifuatiwa na  meneja masoko wa Airtel Dodoma Hendrick Bruno na  wanakikundi wa Pambana wapatao vijana 30 na walezi wa kikundi hicho.
 Mwakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (kulia), akiwa mwenye furaha baada ya kukabidhiwa na Airtel Tanzania, msaada wa pikipiki 2 za  magurudumu matatu aina ya Toyo, malighafi na vifaa mbali mbali vya shughuli za usafi, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika katika eneo lao la biashara Majengo jijini Dodoma hapo jana.Akishuhudiwa na Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki (kushoto),akifuatiwa na meneja masoko wa Airtel Dodoma Hendrick Bruno na Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao.
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kati), akikabidhi vifaa vya usafi kwa mmoja wa wakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (wanne kulia), ikiwa ni sehemu ya msaada wa vifaa vya kufanyia usafi katika jiji la Dodoma, walivyowakabidhiwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, waliopo Majengo  jijini Dodoma hapo jana. Wanaoshuhudia (wane kulia) ni Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao na wanakikundi wa Pambana wapatao vijana 30 na walezi wa kikundi hicho. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
 Diwani wa kata ya Majengo Dodoma, Msinta Mayaoyao (pili kushoto) akitoa maneno machache katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa vya usafi ambapo kikundi cha Pambana kilikabidhiwa  msaada wa pikipiki 2 za  magurudumu matatu aina ya Toyo, malighafi na vifaa mbali mbali vya shughuli za usafi, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, hapo jana. Akisikilizwa na afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kati), Meneja masoko wa Airtel Dodoma Hendrick Bruno (kulia) na wanakikundi wa Pambana wapatao vijana 30 na walezi wa kikundi hicho.
Mwakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (pili kulia) kilichopo Majengo Dodoma akiwa mwenye furaha baada ya kukabidhiwa funguo ya pikipiki aina ya Toyo na afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki, (tatu kushoto), kwa ajili ya shughuli zao za usafi, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika katika eneo lao la biashara Majengo jijini Dodoma hapo jana.
******************
PAMBANA ni kikundi cha vijana 30 wajasiriamali kinachojishughulisha  na shughuli mbalimbali katika jamii kama kukusanya taka, kuzalisha na kusambaza sabuni na kuchomelea vyuma mjini Dodoma, ambao leo wamepokea vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 17 kutoka Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel FURSA. Kundi hili limepokea vifaa mbalimbali vikiwemo pikipiki  mbili aina ya Guta, sare za kufanyia kazi, mabuti, reki ya chuma, ufagio mgumu na  vifaa vingine vya usalama vya kufanyia kazi zao. 

Afisa uhusiano wa Airtel, Dangio Kaniki aliwapongeza kikundi cha Pambana kwa juhudi zao na kufanya kazi kwa bidii. Akizungumza katika hafla ya makabidhiano alisema, " Tumeamua kutoa vitendea kazi vya usafi ili kuweza kuungana na kikundi hiki katika kufikia lengo kuu la kuhakikisha maeneo yanayozunguka jamii yanakuwa katika hali ya usafi na hivyo kuchangia katika mikakati ya kutunza mazingira kwa ujumla.
 
Sambaba na hili Airtel imeona nia na juhudi zao kikundi hiki na ndio maana leo imewakabidhi vifaa vitakavyowawezesha kufanya kazi kwa haraka na kukuza biashara yao". 

"Kikundi cha Pambana kimeshapata mafunzo ya biashara ya ujasiriamali kupitia Airtel FURSA na wataendelea kupata ushauri na uongozi kutoka kwa washauri wa Airtel FURSA ili kuwawezesha kuimarisha biashara yao " aliongeza Kaniki

"Kama kampuni ya simu inayojali jamii yake, tumeahidi  kuwawezesha vijana hapa nchini kwa kuwawezesha kwa njia mbalimbali ili waweze kufikia ndoto zao." alisema Kaniki.

Kwa upande mwingine kundi la Pambana waliahidi  kuweka ujuzi wao wote na kutumia kwa umakini vifaa vilivyotolewa  kwao na Airtel kwa matumizi bora na yaliyo sahihi.

Kiongozi wa kikundi hicho, Amasha Zuberi, aliishukuru Airtel kwa msaada na kutoa wito kwa mashirika mengine hapa nchini  kuuunga mkono mpango wa Airtel katika kusaidia vijana zaidi katika Jamii.

"Hatukuamini siku moja tutakuwa na uwezo wa kufikia malengo yetu katika biashara hii, tunaahidi kuweka juhudi zaidi na kutumia vifaa hivi na mafunzo tuliyopata kwa umakini zaidi kuhakikisha tunainua zaidi biashara yetu," alisema Amasha.

Kwa upande wake, wakati wa hafla ya makabidhiano, Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao alitoa wito kwa vijana kutumia program hiyo ya Airtel Fursa kujiendeleza. Huku akiwaomba watanzania kuwapendekeza vijana wote wanaoona wanafaa kufaidika kwa mradi huo kwa manufaa ya jamii zao kwani Airtel FURSA ipo kwa ajili ya kubadilisha maisha ya vijana hapa nchini.

Airtel FURSA, inazunguka nchi nzima kukutana na vijana kwa lengo la kuwapa elimu ya ujasiriamali na kisha kutoa uwezeshaji kwa vijana ili kuhakikisha kuwa wanafikia ndoto zao.

Ili kijana kushiriki au kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- Jina, Umri, aina ya biashara na eneo.

Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com.  ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, aina ya biashara na sababu ya kuomba msaada kutoka Airtel.
Posted by MROKI On Sunday, May 01, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo