Calvin Martin akimwonyesha Waziri wa Viwanda na
Biashara,Charles Mwijage alipotembelea kiwanda hicho hivi karibuni
Calvin akintembeza Afisa Mwandamizi wa SABMiller Olga
Luskotova alipofanya ziara nchini hivi karibuni.
*********************
WAKATI nchi yetu inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kupiga hatua
kiuchumi na kusababisha wananchi wengi kubaki maskini, wapo baadhi ya
watanzania wana maono kuwa Tanzania inazo fursa nyingi za kuondokana na
umaskini bali tatizo lililopo ni wananchi wengi kutowajibika ipasavyo hususani
katika kufanya kazi wanavyostahili.
Calvin Martin, Meneja wa kiwanda cha kutengeneza Bia cha Tanzania
Breweries kilichopo jijini Dar es Salaam ni miongoni mwa
watanzania wanaoamini kuwa nchi yetu inazo fursa nyingi za kuondokana na
umaskini, kuboresha huduma
za kijamii na wananchi kuishi maisha mazuri.
Ana imani kuwa falsafa ya ‘Hapa Kazi tu’iliyoanzishwa na Rais wa awamu
ya tano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli, ikitekelezwa ipasavyo nchi yetu
itapiga hatua kubwa
kiuchumi kwa kuwa upo ushahidi wa baadhi ya mataifa hususani barani Asia ambayo
kwa kupitia falsafa kama hii wameweza kupiga hatua kubwa kiuchumi kwa haraka.
Katika mahojiano hivi karibuni Calvin alisema kuwa ana imani kuwa mtu
yeyote akifanya kazi kwa bidii na maarifa ni lazima afanikiwe katika jambo
lolote na imani hiyo imemsaidia kufanikiwa katika mambo mengi hadi kufikia hatua alipo ya kuwa Meneja
wa kiwanda cha kutengenezwa vinywaji chini cha Tanzania Breweries. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
“Siku zote naamini kuwa kufanya kazi kwa bidii na ueledi kunaleta
mafanikio na huwa nasikitika sana kuona baadhi ya watu hususani vijana ambao
wanakaa bila kufanya kazi wakati wana nguvu za kutosha na nguvu kazi inapotea bure badala ya kushiriki
katika uzalishaji kwa manufaa yao na manufaa ya taifa”. Alisema.
Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kuwajengea watanzania mazingira mazuri
ya kufanya kazi ziwe
kwa kuajiriwa ama kujiajiri wenyewe na kuongeza kuwa ajira nyingi ziko katika
sekta ya kilimo, ufugaji, viwanda na kwenye ufundi wa aina mbalimbali.
Calvin alisema kuwa amepata elimu ya juu katika Chuo Kikuu Cha Dar es
Salaam ambako alisomea shahada ya kwanza ya Sayansi na alikuwa miongoni mwa wahitimu waliofanya vizuri katika mwaka
1993
Baada ya kumaliza masomo ya Shahada ya kwanza Chuo Kikuu, alijiunga na masomo ya Shahada ya uzamili
chuoni hapo akijikita zaidi katika Sayansi ya viwanda na utawala ambako
alihitimu mwaka 1997.
Ajira yake ya kwanza ilikuwa katika kampuni ya East Africa Breweries
ambako alikuwa kwenye kitengo cha uzalishaji na kwa muda mfupi aliweza kuielewa
fani ya uzalishaji bia kwa vitendo na nadharia, kuhitimu Stashahada ya
utengenezaji bia (Diploma in Brewing) ya Uingereza na baada ya kufanya kazi na
kampuni hiyo kwa miaka mitatu na nusu aliamua kujiunga na kampuni anayofanyia kazi
kwa sasa hivi ya TBL Group.
Akiwa na kampuni hii ameweza kushika nyadhifa mbalimbali hadi kufikia nafasi aliyonayo hivi saa ya
kusimamia kiwanda kikubwa cha TBL Cha Dar es salaam. Moja ya kazi kubwa
anazojivunia nazo ndani ya kampuni hiyo ni kusimamia ujenzi na uanzishwaji wa
kiwanda cha Mbeya.
“Kazi ya kuanzisha kiwanda hiki ilikuwa moja ya changamoto ya kikazi
kwangu lakini
kutokana na ujuzi na uzoefu kwa kushirikiana na wenzangu tulifanikiwa na
najivunia kuona kiwanda hiki ni moja ya viwanda vya kampuni vinavyofanya vizuri
kikiwa chini ya uongozi na wafanyakazi watanzania.
Mbali na kupata elimu za vyuoni akiwa mwajiriwa wa TBL tayari Calvin amehudhuria kozi mbalimbali
ndani ya kampuni ndani
na nje ya nchi ambazo zimezidi kumpatia maarifa ya kitaalamu, kiufundi,
utawala, uendeshaji na usimamiaji wa viwanda kwa ufanisi.
“TBL kuna mafunzo ya aina nyingi na kuna mitambo ya kisasa na mara nyingi
tumekuwa tukipata mafunzo ya aina mbalimbali ikiwemo ya mifumo ya uendeshaji viwanda kwa
ufanisi mfano ‘SABMiller Manufacturing Way’ ambayo tunaitumia na
imeonyesha mafanikio makubwa.
Pia alisema kuna mafunzo ya utawala na mifumo mbalimbali inayowawezesha Mameneja wa viwanda na
wakuu wa vitengo kuendesha shughuli zao vizuri wakiwa wanajua jinsi ya kutoa
vipaumbele kwenye mambo mbalimbali na mpangilio mzuri wa ratiba za kazi.
Calvin aliongeza kusema kuwa anaweza kufanya kazi zake vizuri kutokana
na ushirikiano mzuri anaopata kutoka kwa wafanyakazi wenzake “TBL ni tanuru la
kupika wataalamu na imeajiri watu wenye uwezo mkubwa katika fani zao hivyo
nafanya kazi na wataalamu ambao wana upeo mkubwa na wanaoelewa nini
wanachokifanya, wanaojituma bila kuhitaji usimamizi mkubwa.
Kuhusu changamoto anazokumbana nazo katika kazi yake alisema ni za
kawaida na kutokana na elimu yake na uzoefu wa kazi alionao anaweza kuzitatua
kwa urahisi na maisha kuendela kama kawaida.
Anasema anajivunia
kufanya kazi na kampuni kubwa kama TBL Group ambayo imemuwezesha kujifunza
mambo mengi ikiwemo kupata mafanikio mbalimbali katika maisha yake mojawapo
ikiwa ni kuihudumia familia yake vizuri.
Alimalizia kwa kutoa wito kwa vijana wa kitanzania kutokimbia
masomo ya hesabu na sayansi wanapokuwa mashuleni bali wajitahidi kukomaa nayo
kwa kuwa katika dunia
hii ya sayansi na teknolojia bila wataalamu katika nyanja hii itakuwa vigumu
kwa taifa kupiga hatua ya maendeleo na muda wote wajue kuwa mafanikio
yanapatikana kwa kufanya kazi kwa bidii.
0 comments:
Post a Comment