Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Saidi Meck Sadiki
(kushoto)
na Mkuu wa Wilaya ya Siha Dk. Charles Mlingwa (kulia) wakiwasili katika lango
la Londorosi, Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro. Katikati ni mwenyeji wao Betrita
Loibooki, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro
akiwasilisha taarifa fupi ya Hifadhi ya Kilimanjaro kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Meck Sadiki akiwa
katika lango la Londorosi.
Mkuu wa Idara ya Utalii Hifadhi ya Taifa
Kilimanjaro, Charles Ngendo akionyesha maeneo ya hifadhi kwenye ramani
kufafanua taarifa ya Mkuu wa Hifadhi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Meck
Sadiki akiongea na watumishi wa hifadhi, wilaya na mkoa katika lango la
Londorosi.
Watumishi wa Hifadhi ya Kilimanjaro, Wilaya ya
Siha na Mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro.
Akiongozwa na Mhifadhi Imani Kikoti, Mkuu wa
Mkoa wa Kilimanjaro alipata fursa ya kutembea kwa miguu kupanda mlima kuelekea
uwanda wa Shira.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na ujumbe wake
kutoka mkoani na Wilaya ya Siha wakipewa maelezo juu ya vivutio na jiolojia ya uwanda wa Shira kutoka kwa Charles Ngendo, Mhifadhi Utalii wa
Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro.
Picha ya pamoja ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro alipotembelea
Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro. Hapa akionekana na msafara wake na viongozi wa
hifadhi ya Kilimanjaro wakiwa uwanda wa Shira (mita 3962)
0 comments:
Post a Comment