Timu ya Papo kwa Papo kutoka DW wakiwa katika picha. Kutoka kushoto Daniel Gakuba, Iddi Ssessanga, Grace Kabogo, Sudi Mnette, Bruce Amani na alieketi Caro Robi
Idhaa ya Kiswahili ya DW imeanzisha huduma mpya:
Mukhtasari wa habari ndani ya sekunde 100. Mbali na kukuletea matangazo ya
redio ya kila siku kwa ajili ya Afrika Mashariki na eneo la Maziwa Makuu,
Jumatatu hadi Ijumaa DW itakupatia video fupi zenye habari. Mkuu wa Idhaa ya
Kiswahili, Andrea Schmidt, ana furaha kwamba yeye na timu yake ya waandishi wa
habari kutoka nchi tano tofauti wanaanzisha huduma hii mpya itakayoitwa “Papo kwa
Papo” na
itakayokuwa jicho la kuutazama ulimwengu. Kupitia video zetu utaweza kupata
habari muhimu za kimataifa za kila siku.
“Papo kwa Papo” itapatikana katika chaneli ya YouTube
ya DW Kiswahili, Facebook na toleo fupi la sekunde 60 litarushwa kupitia
WhatsApp.
Miongoni mwa mambo mengine, tutakuletea “hashtag”
zilizovuma pamoja na katuni za kisiasa kutoka kwa wasanii maarufu Gado na Said
Michael.
Pamoja na hayo, kila Ijumaa DW Kiswahili itakuletea
sekunde 100 za matukio muhimu ya kisiasa yaliyotokea katika juma zima.
·
Tafadhali kuwa shabiki wetu YouTube: www.youtube.com/kiswahili
·
Jiunge nasi katika ukurasa wetu wa Facebook: https://www.facebook.com/dw.kiswahili.
·
Pata “Papo kwa Papo” na taarifa zaidi kupitia
WhatsApp. Unaweza kujiunga nasi kupitia kiungo hiki: bit.ly/1Q86kjt
Kila siku Idhaa ya Kiswahili
ya DW inarusha masaa matatu ya matangazo Afrika Mashariki na katika eneo la
Maziwa Makuu. Kwa kushirikiana na redio washirika katika eneo zima, DW
inawapatia wasikilizaji habari zisizoegemea upande wowote kuhusu yanayojiri
duniani kwa ujumla na hasa barani Afrika kupitia masafa ya FM. Ili kutoa
mtazamo huu wa kimataifa, timu ya waandshi wa habari kutoka nchi tano inafanya
kazi na mtandao mkubwa wa waandishi walioko Afrika na kwengineko.
Matangazo ya Kiswahili ni
miongoni mwa matangazo ya DW yenye wasikilizaji wengi zaidi. DW inajumuisha
vipindi vilivyopokea tuzo kama vile Learning by Ear - Noa bongo, jenga maisha
yako - na vipindi vinavyojadili afya, haki za binadamu, mazingira, wanawake na
maendeleo, vijana na utamaduni na sanaa.
www.dw.com/kiswahili
0 comments:
Post a Comment