Nafasi Ya Matangazo

February 28, 2016

 OFISA Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Amanda Fredrick Luhanga (PICHANI), amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia Jumamosi Februari 27, 2016. Taarifa ya kifo cha Bi. Amanda imethibitishwa na Meneja Uhusiano wa TTCL, Bw. Nicodemus Thom Mushi. 

"Ni kweli, Bi Amanda amefikwa na umauti akiwa likizo mkoani Mbeya alikokwenda kuwasalimu ndugu zake.. Aliugua ghafla Alhamisi hii na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya hadi usiku wa kuamkia Jumamosi ambapo Mungu alimchukua," alisema Bw. Thom Mushi. 

 Alifafanua kuwa mwili wa marehemu utasafirishwa siku ya Jumapili, kutoka Mbeya kwenda Njombe na Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu tar 29.02.2016 katika Kijiji cha Mlangali, Ludewa, Mkoa wa Njombe. Mtandao huu unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Bi. Amanda Fredrick Luhanga kwa msiba mkubwa uliowafika. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Apumzike kwa Amani.
Posted by MROKI On Sunday, February 28, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo