Balozi
Modest Jonathan Mero, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa
Mataiafa na Mashirika mengine ya Kimataifa Geneva na Vienna akiwasilisha
hotuba ya Tanazania katika mkutano mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa
la Viwanda Duniani ambao unajadili maendeleo endelevu ya viwanda kama
njia mbadala ya kuzikwamua nchi maskini. Mkutano huu unafanyika jijini
Vienna, Austria kuanzia tarehe 30 Novemba hadi tarehe 4 Desemba 2015.
Katika
hotuba yake, Mhe. Balozi Mero, pamoja na mambo mengine aliwaleza
wajumbe wa mkutano huo hatua mbali mbali ambazo zimekuwa zikichukuliwa
na Serikali ya Tanzania kwa lengo la kukuza viwanda nchini ikiwa ni
pamoja na mafanikio ambayo yamefikiwa hadi sasa.
Mhe.
Balozi Mero pia alizungumzia juu ya mapitio ya Mpango wa Kitaifa wa
Maendeleo wa awamu ya pili (National Development Plan Phase Two) ambao
utatekelezwa na Serikali kuanzia 2016/2017 hadi 2020/2021 ambao pamoja
na mambo mengine umeweka msisitizo wa kukuza viwanda kwa lengo la
kuongeza thamani ya rasimali zetu, kukuza mahitaji ya ndani ya bidhaa za
viwandani na kuongeza ajira kupitia viwanda, Sekta nyingine za
uzalishaji, huduma duniani.
0 comments:
Post a Comment