Mwanamuziki Fid Q akitoa burudani
katika moja ya tamasha la Coke Studio
Wanafunzi kuanzia shule za msingi
nchini hadi vyuo vikuu wameshiriki kuonyesha vipaji vyao katika msimu huu wa
Coke Studio kama wanavyoonekana katika moja ya tamasha la Coke Studio.
Wasanii wa muziki wakitoa burudani
katika moja ya tamasha la Coke Studio mkoani Mwanza
Mwanamuziki Ali Kiba na Victoria
Kimani wakiwa katika onyesho la Coke Studio.
**************
Onyesho la Coke Studio msimu wa tatu linaloendelea linazidi kuleta
burudani na furaha kwenye makundi mbalimbali ya jamii na kuacha gumzo kwa wengi
nchini.
Vijana wengi wameeleza kuwa pamoja na kuburudika na maonyesho ya kolabo za wanamuziki machachari
yanayoonyeshwa kupitia luninga ya Clouds kila siku ya Jumamosi na kwenye redio
ya Clouds bado wamekuwa wakipata burudani kutoka matamasha shirikishi
yanayoendelea kwenye mikoa mbalimbali na kushirikisha watu kutoka makundi
mbalimbali ya jamii.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali walipohojiwa juu ya onyesho hili
walisema kuwa linaleta raha na burudani huku likiibua vipaji na kuwakutanisha
vijana na watu wanaojiamini ambao wamefanikiwa kwenye mambo wanayoyafanya. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
“Coke Studio ni zaidi ya burudani kwa kuwa pia inatuwezesha vijana
kuonyesha vipaji wakati huo huo kukutana na watu ambao wanajiamini ambao
wamefanikiwa katika mambo yao”.Alisema Willy Chale Mwanafunzi wa Sekondari ya
Mwanza.
Miriam Chande mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa fedha alisema
analipenda onyesho la Coke Studio kwa kuwa linatoa burudani ya aina yake ya
muziki ambayo imewalenga vijana na inawawezesha kupata jumbe za kuwahamasisha
kusonga mbele kimaendeleo.
Kassim Juma,mwendesha bodaboda na mwanamuziki wa kujitegemea amesema
kuwa yeye na wenzake wanapenda onyesho la Coke Studio kwa kuwa ni la viwango na
limelenga kutoka burudani kwa makundi
mbalimbali kupitia kuangalia kolabo za wanamuziki na matamasha ya muziki na
burudani yanayoendelea sehemu mbalimbali nchini.
Msimu wa Coke Studio mwaka huu umeshirikisha wanamuziki mbalimbali
kutoka Tanzania na nchi za nje
Wanamuziki hao ni Fid Q ambaye amefanya kolabo (mash-up) na Maurice
Kirya na Vanessa Mdee ambaye amefanya kolabo (mash-up) na mwanamuziki 2face
kutoka Nigeria , Ali Kiba na Victoria
Kimani na Ben Paul na wangechi.
Msimu huu wa Coke Studio umeambatana na kampeni mpya yenye jina la
‘Sababu Bilioni za Kuamini’, na hivyo kujumuisha vijana mbalimbali ambao
wanaamini katika kufikia malengo yao bila ya kujali changamoto zinazowakabili.
Lengo kuu la Coke Studio Afrika ni kuwakutanisha kwa pamoja wasanii
wenye mbalimbali wa Afrika na kuimba nyimbo ambazo zina vionjo tofauti hivyo
kuongeza msisimuko. Lakini vilevile kutoa fursa kwa wasanii wachanga kushirikiana na wakubwa ili kuwapa changamoto
ya kuongeza ujuzi katika kazi zao na kuzidi kukuza vipaji vyao
0 comments:
Post a Comment