Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick (kushoto) akimkabidhi msaada wa
madawa ya kusafishia maji yaliyotolewa na Benki ya DCB kwa Mkurugenzi wa
Manispaa ya Kinondoni, Musa Natty, Dar es Salaam jana. Katikati ni Meneja
Mwandamizi ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Gray Ndandika. DCB
walikabidhi madwa yenye thamani ya shilingi milioni tano kwaajili ya
kukabiliana na ugonjwa wa kindupindu. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB, Balozi Paul Rupia. Benki ya DCB ilikabidhi katoni 58 za dawa zenye thamani ya shilingi Milioni 5.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick (kushoto) akimkabidhi msaada wa
madawa ya kusafishia maji yaliyotolewa na Benki ya DCB kwa Mkurugenzi wa
Manispaa ya Kinondoni, Musa Natty, Dar es Salaam jana. Katikati ni Meneja
Mwandamizi ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Gray Ndandika. DCB
walikabidhi madwa yenye thamani ya shilingi milioni tano kwaajili ya
kukabiliana na ugonjwa wa kindupindu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB, Balozi Paul Rupia akizungumza katika makabidhiano hayo ambapo alisema Benki hiyo imetoa msaada huo kwa kuguswa na tatizo la mlipuko wa kipindupindu unaoikabili wilaya ya Kinondoni na hivyo kuitikia wito na ombi la Mkurugenzi wa Manispaa kutoa madawa ya kusafisha maji ili kukabiliana na ugonjwa huo. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa
Manispaa ya Kinondoni, Musa Natty (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadicky (wapili kulia) na Meneja
Mwandamizi ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Gray Ndandika.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadicky akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo Dar es salaam leo ambapo aliwashukuru Benki ya DCB kwa msaada huo na kuzitaka taasisi zingimne kuiga mfano huo. Aidha aliwataka watendaji wa Kata kuwa makini na kazi zao na kuhakikisha ugonjwa huo unatokomezwa katika maeneo hayo na watu wakaidi wa kufuata kanuni za usafi kuchukuliwa hatua.
Baadhi ya watendaji wa Kata mbalimbali za Manispaa ya Kinondoni wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa na viongozi wengine wakati wa makabidhiano hayo.
0 comments:
Post a Comment