Mwanamuziki wa Muziki wa kizazi kipya Maarufu
kama bongo fleva KLEYAH ambaye anakuja kwa kasi katika Tasnia hiyo hatimaye amezindua nyimbo yake mpya
inayokwenda kwa jina la MZOBE MZOBE wimbo aliomshirikisha msanii maarufu maarufu kutoka THT Barnaba Boy CLASSIC nyimbo
ambayo inatabiriwa kufanya vizuri katika soko la musiki wa Tanzania.
KLEYAH ambaye ni Mhitimu wa shahada ya mawasiliano kutoka chuo kikuu cha
cha Phoenix nchini marekani na baadae kufanya kazi katika shirika la kimataifa
la UNDP kabla ya kuacha na kuamua
kurejea nchini kwa ajili ya kuendeleza na kukuza sanaa yake Tayari amefanikiwa
kufanya kazi na watayarishaji na wasanii wakubwa ambapo mwaka 2014 alifanikiwa
kufanya nyimbo mbili ambazo zilirekodiwa nchini Kenya na mtayarishaji maarufu nchini
humo Lucas Bikedo pamoja na kufanyia Video kwa watayarishaji maarufu nchini
Kenya kwa sasa OGOPA DJS.
Katika nyimbo yake mpya ambayo ilizinduliwa Tarehe 6 Mwezi November na kuchezwa
katika vituo mbalimbali vya Radio nchini Tanzania na Africa mashariki kwa
ujumla na hatimaye leo umefanyika uzinduzi wa Video yake ya wimbo wa MSOBE
MSOBE unataraji kutambulishwa katika vituo mbalimbali vya Televission kwa ajili
ya kumtambulisha msanii huyo ambaye anaonekana kuja kwa kasi katika sanaa hii
ya music wa kizazi kipya.
Akizungumza nara Baada ya uzinduzi wa Video yake msanii KLEYAH amesema kuwa
kwa sasa mipango yake ni kuendelea kufanya kazi pamoja na watayarishaji wakubwa
nchini Tanzania pamoja na wasanii maarufu ili kukamilisha album yake ambayo
amepanga kuizindua mwezi July mwaka 2016 album ambayo ametamba kuwa itasheheni
aina mbalimbali za misic ili kuwafurahisha mashabiki wanaofwatilia kazi zake.
Ameongeza aliamua kufanya music kwa kuwa ni kitu ambacho kipo ndani ya moyo
wake huku akieleza kuwa kusoma na baadae
kufanya music ni jambo la kuigwa na wasanii wa Tanzania kwani itamsaidia msanii
kutoboa tu si ndani ya nchi lakini Barani Africa na duniani kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment