Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akimkabidhi
vifaa vya michezo Mwenyekiti wa timu ya waandishi wa habari za michezo nchini
(Taswa SC) Majuto Omary kwa ajili ya kutumika katika mechi zao.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akimkabidhi
vifaa vya michezo moja wa wachezaji wa timu ya netiboli ya waandishi wa habari
za michezo nchini (Taswa Queens), Imani Makongoro kwa ajili ya shughuli zao mbalimbali za
michezo. Anayeshuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary
************
Kampuni ya Airtel Tanzania imeiipiga ‘tafu’
timu ya soka na netiboli ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa SC kwa
kuwapatia vifaa vya michezo.
Akizungumza katika makabidhiano hayo jana, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson
Mmbando alisema kuwa kampuni yao inatambua mchango wa waandishi wa habari za
michezo nchini katika kuendeleza michezo na kuamua kutoa vifaa vya michezo
ambazo ni seti mbili za jezi na mipira. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Mmbando alisema kuwa mbali ya kuwa wadau wakubwa wa michezo,
msaada huo ni moja ya muendelezo wao katika shughuli za kijamii.
“Airtel Tanzania ni wadau wakubwa wa michezo na burudani,
tumeshiriki katika shughuli mbali mbali ikiwa kuendesha michezo ya Airtel
Rising Stars, tumeamua kuunga mkono juhudi za timu ya waandishi wa habari za michezo kuwakutanisha wana-habari na kushiriki katika mazoezi na
mechi kwa ajili ya kuhamasisha vipaji na afya zao,” alisema Mmbando.
Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliishukuru Airtel Tanzania
kwa msaada huo ambao umetokana na maombi yao kwa kampuni hiyo. Majuto alisema kuwa Taswa SC kwa kujua wadau wake, waliamua kuomba
msaada wa vifaa hivyo na Airtel Tanzania kuwajali na kuchukua juhudi za haraka kutoa
mchango wao.
“Tumeomba kwa kampuni
nyingi, bado hatujapata majibu ya
kukubaliwa au la, Airtel Tanzania imeonyesha mfano kwa kutusaidia kwa haraka
sana, ni faraja kwetu, tunawaomba wengine waige mfano wao,” alisema Majuto.
Alisema kuwa Taswa SC bado inakabiliwa na changamoto ya vifaa
vingine kama viatu kwa timu zake za soka na netiboli na kuwaomba wadau wafikirie
kuwasaidia. “ Tupo tayari kupokea vifaa vingine, timu inatakiwa kuwa na vifaa vya kutosha, jezi za aina mbalimbali,
mipira ya mazoezi na mechi, hivyo kama kuna wadau wanataka kutusaidia, wasisite
kufanya hivyo,” alisisitiza Majuto.
0 comments:
Post a Comment