Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Profesa John Nkoma akifungua mkutano na waandishi wa Habari na kuzungumzia umuhimu wa kusajili namba za simu za Mkononi na Mfumo mpya wa kusajili namba na kuhakiki kutumia Teknolojia mpya ya Kielekroniki.
Mwenyekiti wa umoja wa makampuni ya mawasiliano Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bwana Rene Meeza akitamka Rasmi Uzinduzi wa usajili mpya wa simu za mikononi kwa kutumia Teknolojia mpya ya kutumia smart phone kutumia Programu ya KYC
Muwezeshaji katika mkutano na waandishi wa habari, Isack Mruma akifafanua jambo
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi hati wa NIDA Thomas William
akizungumza umuhimu wa kuwa na kitambulisho cha Taifa ambapo ndicho
kitakuwa kitambulisho rasmi katika kusajili Namba mpya za simu na
kuhakiki kwa wale ambao tayari wamejisajili.
Mfumo mpya wa Kielekroniki kutumia Smart Phone kwa Program ya KYC inavyofanya kazi.
***********
***********
Mfumo mpya wa Usajili wa Namba za Simu (Sim Card registration) kwa kutumia Teknolojia mpya ya Kidijitali Kupitia Smart Phone kwa Programu ya KYC umezinduliwa Rasmi leo Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ukiwahusisha Makampuni ya simu, NIDA, Polisi na TCRA.
Akizungumza
katika Mkutano huo wa uzinduzi wa Huduma hiyo ya kisasa Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma amesema kuwa mwanzo
kulikuwa hakuna changamoto sana juu ya laini za Simu lakini kwa sasa
zaidi ya laini za simu 32,000,000 zilizo sajiliwa, Pia alizungumzia
umuhimu wa kujisajili ikiwa ni pamoja kwa usalama, kutunza amani pia
kusaidia mamlaka kuwa na kumbukumbu za watu ambao wamejisajili..
Nae
Mwenyekiti wa umoja wa makampuni ya mawasiliano Tanzania ambaye pia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bwana Rene Meeza alielezea kwa
kina namna ya mfumo huo mpya utakavyofanya kazi ambapo katika usajili
mpya wa Kielekrinki kutakuwa na kusajili kwa kutumia kitambulisho cha
Taifa ambapo zoezi kupata vitambulisho vya Taifa kwa wananchi Tanzania
Linaendelea.
Alielezea
Mfumo huo mpya wa Sim Card registration kuwa unakwenda kwenda kwa
kutumia Smartphone ambayo itakuwa na Programu ya KYC ambapo mteja
atasajiliwa ndani ya simu hiyo kuanzia kuandika Majina yake, Atapigwa
Picha, Kitambulisho chake kitapigwa picha kama ni Feki Mashine Simu
haita kipiga picha, pia Mteja ataweza kutia Saini yake pale pale kwenye
simu. Aliongeza kuwa Mfumo huo utapatikana kwa Mawakala wa Makampuni
husika wa Simu za mkononi.
Alimalizia kwa kusema kuwa Mfumo huo mpya
utatumika kwa kuanza kusajili namba mpya za simu kwa Kutumia
kitambulisho cha Taifa kama ndio Kitambulisho Rasmi ingawa viambulisho
vyengine kama Hati ya kusafiria itaweza kutumika, Pia mfumo huo
utatumika kuhakiki Namba za simu ambazo tayari zimesajiliwa.
Pia
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi hati wa NIDA Thomas William
alizungumza umuhimu wa kuwa na kitambulisho cha Taifa na Kushukuru
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania pamoja na Makampuni ya Simu kwa
kuanzisha Mfumo huo mpya ambao utarahisisha kazi na kuongeza ufanisi
zaidi. Story na Blogs za Mikoa.
0 comments:
Post a Comment