Mke wa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakia Bilal, akimfariji
mke wa aliyekuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Marehemu Shaaban Issa Bin Simba, Bi
Makaje Goso, wakati alipofika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, leo
Juni 16, 2015 kwa ajili ya kuifariji familia hiyo kabla ya kusafirisha mwili wa
marehemu kuelekea nyumbani kwake Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya maziko
yanayotarajia kufanyika leo jioni. Kushoto ni Makamu wa Rais Dkt. Mohammed
Gharib Bilal.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed
Aboud Mohammed, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Ofisi za Bakwata,
Kinondoni kwa ajili ya kuhudhuria Kisomo cha Marehemu Simba, leo Juni 16, 2015.
Katikati ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akishiriki na baadhi ya Viongozi katika Kisomo cha kumuombea Marehemu Mufti
Shaaban Bin Simba, kilichofanyika leo Juni 16, 2015 kweny Viwanja vya Ofisi za
Bakwata zilizopo inondoni, jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akishiriki swala maalumu ya kuswalia Jeneza (halipo pichani) na baadhi ya
viongozi wa kitaifa wakati wa kisomo maalumu kilichofanyika leo Juni 16, 2015
kwenye Viwanja vya Ofisi za Bakwata zilizopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam,
kwa ajili ya kumuombea marehemu.
0 comments:
Post a Comment