JUNI 16 ya kila mwaka bara
la Afrika huadhimisha siku ya mtoto wa
Afrika ikiwa ni tukio la kuwaenzi na kuwakumbuka watoto wa Soweto nchini
Afrika Kusini waliofariki wakati wa maandamano ya kutaka haki na usawa katika
elimu kutoka utawala wa Makaburi mwaka 1976.
Ni Umoja wa Nchi huru za
Afrika (OAU) hivi sasa Umoja wa Afrika (AU) mwaka 1991 ndio waliamua kuifanya
siku hiyo kuwa ya kuwakumbuka na kuwaenzi wa watoto wa Afrika kwa maadhimisho
ya kitaifa na kimataifa ambayo yanafanyika kwa kuzungumzia haki za mtoto.
Huu ni mwaka wa 24 tangu
AU iidhinishe siklu hiyo ya mtoto wa Afrika kuadhimishwa, lakini pia ni mwaka
wa 39 tangu watoto wa Soweto wapoteze maisha yao wakati wakidai haki yao.
Mwaka jana maadhimisho
hayo yalikuwa na kaulimbiu ya “Haki ya Ushiriki: Waache watoto waonekane na
wasikike” na mwaka huu pia kuna kauli mbiu yake ambayo inaogoza maadhimisho
hayo hii leo.
Pia maadhimisho ya mwaka
huu yanafanyika wakati Wakuu wa Nchi za Afrika chini ya Umoja wao AU wanakutana
nchini Afrika kusini ambapo miaka 39 iliyopita palitokea vuru na watoto
kuuwawa.
Siku ya Mtoto wa Afrika
mwaka huu inafanyika sambamba na
maadhimisho ya Miaka 25 ya Kupitishwa kwa Mkataba wa Haki za Mtoto wa Afrika na
kaulimbiu ya mwaka huu ni: “Kuongeza Kasi na Jitihada Zetu za Pamoja Kutokomeza
Ndoa za Utotoni Afrika.”
Kama mzazi ambaye nami ni
nawatoto wa kike na hata wakiume pia ninaunga mkono kauli mbiu ya mwaka huu.
Mimba za utotoni katika
nchi nyingi za Afrika bni tatizo kubwa ambalo hakika linahitaji sauti ya pamoja
ya kulikemea ili kuliondoa kama si kulimaliza kabisa.
Vita vya mara kwa mara
katika nchi nyingi za Afrika ni moja ya vitu ambavyo husabisha watoto wengi wa
kike kupata mimba za utotoni kutokana nakubakwa na hata wengine kunajisiwa.
Lakini hapa Tanzania sisi
tuna amani ya kutosha na utulivu ambao kama tutautumia ipasavyo hili tunaliweza
kuliondoa achilia mbali umasikini unaozikabili kaya zetu na kupelekea watoto
hasa washule kulubuniwa na malaghai wachache na kuishia katika mimba.
Lakini wapo wazazi
waliokosa hekima na busara ambao huwaoza binti zao wakiwa na umri mdogo na
wengine hata bila kuwashirikisha watoto hao.
0 comments:
Post a Comment