Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Chato ikiwa siku yake ya kwanza ya ziara mkoani Geita baada ya kumaliza ziara ya siku 10 mkoa wa Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM anazunguka nchi nzima kukagua,kuhimiza na kusukuma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
Umati wa wakazi wa Chato mjini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia kwenye uwanja wa stendi ya Zamani.
Katibu Mkuu wa CCM aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali inabidi ifute kodi kandamizi zinazowazuia wananchi kurahisisha maisha yao.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Chato mjini.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akihutubia wakazi wa Chato mjini ikiwa siku ya kwanza ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mkoani Geita.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi kwa mwanachama mpya wa CCM, zaidi ya wanachama 361 wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi na kukabidhiwa kadi zao leo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Umati wa wananchi wa Chato mjini wakishangilia mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliyeanza ziara ya siku sita mkoani Geita.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa kutoka wilaya ya Chato akihutubia kwenye mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa stendi ya zamani ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Diwani wa Kata ya Nyamirembe Ndugu John Ibawa akimuelezea matatizo ya maji pamoja na matatizo ya ardhi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyiaka katika kijiji cha Kazunguti,mkoani Geita.
Bw.Shambinga David akielezea uhitaji wa umeme katika kijiji chao cha Makugusi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo mkoani Geita kwa ziara ya siku 6 ya kuhimiza, kukagua na kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akigonga tano na wakazi wa kijiji cha Makurugusu mara baada ya kujibu hoja yao ya msingi ya matatizo ya umeme.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Diwani wa kata ya Biziku Bw. Magomamoto Zanzibar akijinadi na kueleza namna alivyotekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM katika kata yake.
0 comments:
Post a Comment